Grumeti Fund imeajiri zaidi ya wafanyakazi mia moja, kulinda, kusimamia na kuangalia rasilimali na wanyamapori katika mapori ya akiba ya Grumeti. Tunawashukuru kwa ari na kujitoa kwao kwani kumepelekea wanyamapori kuongezeka tena tofauti na ilivyokuwa yapata miaka kumi iliyopita. Sasa makundi makubwa huonekana katika maeneo haya yenye kuvutia kipindi cha uhamaji wa wanyamapori wa kila mwaka. Haya ni matokeo ya moja kwa moja ya timu yetu kulinda kwa uthabiti na kuimarisha tena ikolojia hii iliyoko hatarini.