Grumeti Fund

Grumeti Fund ni Shirika lisilo la faida linalochangia kuhifadhi Ikolojia ya
Serengeti kwa vizazi vijavyo.

TAZAMA VIDEO KAMILI

Kazi zetu

Sehemu nyingi ulimwenguni zinapoendelea kuharibika kutokana na ongezeko kubwa la watu, Grumeti Fund kwa kushirikiana na washirika wetu wa Tanzania inajizatiti katika kuhifadhi ekari 350,000 za eneo la Magharibi mwa Serengeti zilizopuuzwa hapo awali. Kupitia usimamizi dhabiti wa uhifadhi, kushirikiana na jamii, ubunifu wa teknolojia na kutumia askari mahiri tunaleta mabadiliko chanya na matokeo endelevu ya uhifadhi.

front

Ripoti ya Matokeo 2021

“Mafanikio endelevu ya uhifadhi wa maeneo ya magharibi mwa Serengeti ni matokeo ya pande mbili ya kulinda wanyamapori na kuboresha maisha ya jamii za pembezoni mwa maeneo haya.”

Pakua

Miradi muhimu

Mafanikio ya kazi za uhifadhi na kuboresha maisha ya jamii za pembezoni zinazofanywa na Grumeti Fund hutegemea uhisani wa wafadhili. Mchango wako utasaidia kuendelea kuhifadhi maeneo haya muhimu ya Ikolojia ya Serengeti na kusaiidia maendeleo ya jamii za pembezoni.

Changia

Habari Mpya

Fuatilia baadhi ya nyakati zetu nzuri zaidi za nyuma ya pazia na endelea kuhabarika na Habari zetu mpya na baadhi ya makala zenye taarifa kedekede hapa chini.

  • Kutafakari Miaka Mitano ya Women in the Field

    Katika Siku hii ya Kimataifa ya Wanawake tunafuraha kusherehekea sio tu mafanikio makubwa ya wanawake duniani kote lakini pia hatua muhimu ya miaka 5 ya mpango wetu wa Women in the Field (WIF). Tulipozindua mpango wa Women in Field (WIF) mwaka 2019, tulilenga kukuza taaluma......

  • Kuwawezesha Walinzi wa Wanyamapori

    Askari wetu waliojitolea kupambana na ujangili walipitia programu ya kuboresha ujuzi wao mwezi Januari. Chini ya uelekezi wa Simon Leaks kutoka Big 5 Protection, mafunzo haya maalum ya ujuzi wa kufuatilia yalilenga kuinua uwezo wao wa kulinda wanyamapori kwa viwango vya juu. Simon alisisitiza jukumu......

  • Kustawi Zaidi ya Biashara na Programu ya RED ya Grumeti Fund

    “Nilikuwa nikifikiri elimu hukoma baada ya shule, lakini sasa nafahamu ni safari ya maisha yote” analisema akiwa na shauku ya hekima mpya. Hata wazee kama sisi wanaweza kuendelea kujifunza na kukua. Mpango huu uliniongeza ubunifu na ujuzi wangu wa kufikiri – ni zaidi ya biashara......

Makala zaidi

Washirika wakuu

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia