Miradi Maalumu

Kwa kushirikiana na idara nyingine, Idara ya miradi maalumu hufanya kazi kama kichochezi cha nguvu kati ya Grumeti Fund. Kutambulisha teknolojia mpya na mbinu za kibunifu za uhifadhi, uzuia-ujangiri na tafiti na ufuatiliaji, kuwezesha shirika kupata matokeo mazuri na ya uhakika kuleta yenye mafanikio makubwa.

Miradi maalumu iliyowekwa hujumuisha kitengo cha mbwa, DAS, ndege zisizokuwa na rubani, kamera za siri za TrailGuard na uwekwaji wa kola za GPS kwa tembo. Miradi mingine chini ya Idara ya miradi maalumu ni programu ya Grumeti Fund ya uongezaji wa faru weusi, utambulishaji mpya wa tandala mkubwa na programu muhimu ya msaada wa anga.

Teknolojia ya Uzuia-Ujangiri

Mfumo wa Ufahamu wa Kikoa (DAS)

Taarifa hujazwa mara moja kwenye kanzidata na timu zetu za uhifadhi, utafiti na ufuatiliaji na utekelezaji wa sheria zinazofanya kazi kwenye eneo letu lote. Taarifa hizi huweza kupatikana kwa wakati muafaka na kutafsiriwa kuwa taarifa zenye manufaa zinazowawezesha mameneja kutoka idara husika za Grumeti Fund kufanya maamuzi bora ya kiusimamizi. Matumizi ya wakati muafaka wa kanzidata. Hili limeboresha zaidi jitihada zetu za kulinda maeneo haya yenye mandhari nzuri ya kiikolojia magharibi mwa Serengeti.

SOG accomodation, Store room, OPS Room, Canine unit, Armery room_101 Resized

Programu ya ndege za uchunguzi zisizokuwa na rubani

Ndege za uchunguzi zisizo na rubani zina programu ya utambuzi wa picha na video. Ndege isiyokuwa na rubani huruka kwenye gridi zilizowekwa awali na kuchukuwa picha za video. Programu ya utambuzi wa picha imetengenezwa kuweza kuchagua na kutofautisha vitisho vyenye uwezekano kama vile majangiri na mifugo na wanyamapori. Kama kitisho chenye uwezekano kikitambuliwa, video fupi huripotiwa kwa ajili ya mtaalamu wa chumba cha ops kuipitia picha.

 

Pindi kitisho kinapo thibitishwa, Mfumo wa Ufahamu wa Kikoa (DAS) usajili hii taarifa kwa wakati muafaka na rasilimali za utekelezaji wa sheria hutumwa mara moja kukabili tatizo.

Drones - 1[1] Resized

Kikosi cha Mbwa

Kitengo cha Mbwa cha Grumeti Fund ni kitengo cha askari na mbwa wenye uwezo wa kunusa na kutambua changamoto hifadhini ambacho hutusaidia kuwa hatua moja mbele ya majangiri. Uwepo wa kudumu wa mbwa wetu wa ukombozi wanne – Tony, DJ, Radar na Popo – na waangalizi wao wenye stadi huongeza uwezo wa idara ya Uzuia-Ujangiri wa kukamata majangiri.

Grumeti Fund inatazamia kutumia Kitengo cha Mbwa kwenye Ikolojia ya Serengeti yote, kwa kushirikiana na mashirika ya kiserikali na yasiyokuwa ya kiserikali ya kihifadhi kuongeza matokeo. Kwa hakika, tunaona mbwa wakifanya kazi kuwazuia majangiri kuingia katika eneo la hifadhi kikamilifu.

special projects header Resized
research-and-monitoring_wildlife_translocation_projects

Programu maalumu

Grumeti Fund imejizatiti kuleta mchango wenye maana kwenye kuongeza idadi na ulinzi wa Faru mweusi aliye hatarini wa Afrika Mashariki ndani ya Ikolojia ya Serengeti. Kwa kushirikiana bega kwa bega na wadau wetu katika serikali ya Tanzania, tuna wahamisha na kuwatambulisha upya faru Weusi kwenye mazingira yao ya awali ya nyanda za juu kaskazini mwa Tanzania.

Soma zaidi

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia