MIRADI YA GRUMETI FUND INAYOHITAJI UHISANI 2024.

Grumeti Fund inategemea ukarimu wa wafadhili kuweza kufanya programu zetu za uhifadhi na kijamii. Ni kwa ukarimu wa wafadhili wetu tunawezakufanya kitu chochote. Kwa hili, tunakushukuru sana kwa mchango wako.

Programu ya msaada wa kufundisha -Gharama za uendeshaji kwa mwaka $250,000

 

Elimu ya awali na msingi ni muhimu kwa kuwa huwajengea watoto wetu msingi imara wa maisha yao ya baadaye. Ufundishaji bora na kujifunza kwa ufanisi nje na ndani ya darasa hutegemea kwa kiasi kikubwa walimu wazuri kama wajenzi wa msingi huo. Vilevile kuwa na uwiano mzuri wa walimu na wanafunzi ni muhimu ili kuhakikisha malengo ya zoezi la kujifunza hufanikiwa. Kwa bahati mbaya, mahitaji haya muhimu hayatolewi kwenye shule nyingi zilizoko kwenye vijiji vinavyopakana na maeneo yetu ya hifadhi. Idadi ya walimu kulinganisha na wanafunzi ni ndogo, na baadhi ya shule walimu ni wachache sana, – ni changamoto kubwa ambayo huathiri matokeo mazuri ya kujifunza na kufundisha.

Programu ya Msaada wa Kufundisha (TSP) ya Grumeti Fund hutatua changamoto hii kwa kuwapeleka vijana 52 wenye ari, na waliohitimu elimu ya chuo kikuu kwenye jumla ya shule za msingi 26 ili kuongeza uwiano wa walimu na wanafunzi ambao utaboresha mafanikio ya kitaaluma ya wanafunzi na uwezekano wao wa kutambua ubaadaye wao.

Msaada wa operasheni za anga – $50,000

 

Gharama za uendeshwaji wa ndege kwa ajili ya shughuli za kukabiliana na ujangili na tafiti na ufatiliaji.

Msaada wa operasheni za anga – $50,000

 

Gharama za uendeshwaji wa ndege kwa ajili ya shughuli za kukabiliana na ujangili na tafiti na ufatiliaji.

Kazi za skauti wa hifadhi – Gharama za kuhudumia skauti 80 kwa mwaka $ 365,000

Kikosi cha skauti cha Grumeti Fund kinaundwa na maskauti 80 waliosambazwa kimkakati kwenye kambi kumi na mbili za skauti katika maeneo ya hifadhi. Ongezeko la idadi ya wanyamapori kwenye maeneo yetu unathibitisha ufanisi wao. Ili kuwawezesha skauti kufanya kazi zao kwa ufanisi na kwa usalama iwezekanavyo ina maana kuwapatia vifaa vinavyostahili – GPS, redio, sare, huduma ya kwanza, magari, pamoja na kuhakikisha wanaishi katika makazi bora na wanakula vyakula vya lishe kwa kiwango kinachostaili. Zaidi ya mahitaji haya ya kila siku, pia ni muhimu maskauti wapewe mafunzo ili kuweza kukabiliana na dharura za kimatibabu pamoja na mbinu za ulinzi binafsi, mafunzo kutumia silaha na kadhalika.

1. Mishahara ya mwaka kwa skauti 80 – $300,000
2. Gharama za mafunzo ya mara kwa mara kwa mwaka – $40,000
3. Gharama za vifaa vya maaskari kwa mwaka – $15,000
4. Gharama za sare za maskauti kwa mwaka – $10,000

Uhisani

 

Kwa mwaka mmoja shule za sekondari $1,300

Kwa mwaka mmoja kwenye vyuo vya ufundi stadi $4,500

Ustawi wa wanyamapori

 

Gharama ya kumtoa mtego mnyama mmoja $300

Wahitimu wa chuo kikuu – $ 84,000

 

Hapa RISE tunapambana kuunganisha tafiti za kisayansi na uhitaji wa menejimenti huku tukitoa fursa kwa kizazi kijacho cha watanzania wahifadhi. Moja ya njia muhimu ya kufikia haya malengo ni kwa kuwasaidia watanzania ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu ndani na nje ya nchi kufanya tafiti kwenye mada zenye uzito magharibi mwa Serengeti. Kwa sasa wahitimu wa vyuo vikuu husoma uchumi, ikolojia, gharama na faida za kuwa na fensi ya umeme, tabia za kutawanyika kwa tembo na masuala yanayoathiri kuzaliana kwa tai. Tunatarajia kuwasaidia wahitimu wa vyuo kufanya miradi kwenye utafiti wa magonjwa ya wanyamapori , kupambana na mimea vamizi, na kutathmini jitihada za urejeshaji wa vyanzo vya maji katika hali yake.

1. Hisani warsha ya ana kwa ana ya uandishi kwa watahiniwa 10 waotazawamiwa kuendelea na masomo – $6,000
2. Saidia kununua mashine ya PCR kwa ajili ya maabara yetu – $6,000
3. Saidia mhitimu wa chuo kikuu anaeendelea na masomo kwenye chuo cha kitanzania kwa mwaka mmoja – $12,000
4. Saidia mhitimu wa chuo kikuu anaeendelea na masomo kwenye chuo cha kimataifa kwa mwaka mmoja – $60,000

Kamera za wanyamapori – Gharama za uendeshaji kwa mwaka $7,500

 

Changia kamera moja – $200

Tusaidie kangalia spishi za wanyama waliohatarini kutoweka kama vile faru mweusi, kima “patas monkey”, na spishi hadimu kwenye maeneo haya kama korongo, swala na tandala.

Kituo cha Elimu ya Mazingira – Gharama za uendeshaji wa kituo kwa mwaka $100,000

 

Lengo la Grumeti Fund kwenye elimu huangazia hadi kwenye mazingira na wajibu wa kila mtu kupunguza madhara kwenye rasilimali chache tulizonazo duniani. Kwenye Kituo cha Elimu ya Mazingira (EEC), wanafunzi ambao huambatana na walimu wao hujifunza masuala nyeti ya kimazingira kama vile ukataji wa miti, mmomonyoko wa udongo na utunzaji wa vyanzo vya maji, masuala haya huathiri kila mmoja. Mwaka 2023, tunategemea kuwa na wanafunzi 480 kutoka shule za sekondari 15 tofauti. Ni muhimu tusambaze kwa kasi ujumbe wa umuhimu wa kutunza mazingira na mchango mkubwawa jamii kwenye kuhakikisha mimea na wanyama wa taifa lao hudumu kwa muda mrefu. Kiwango hiki kitakidhi gharama za uendeshaji za EEC kwa mwaka mmoja.

Kuwavisha tembo kola – Gharama za uendeshaji kwa mwaka $60,000

 

Saidia kuvisha kola moja – $5,000

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia