Uzuiaji ujangiri na utekelezaji wa sheria

Matukio mengi ya ujangiri Grumeti uhusisha ujangiri wa uuzaji wa nyamapori, ingawa, ujangiri wa tembo kwa ajili ya pembe uko palepale na unaweza kuongezeka. Grumeti Fund hujumuisha teknolojia pamoja na askari mahiri kudhibiti uwindaji huu wa pande mbili. Tumeweka kambi kumi na mbili za kudumu za askari wa doria na mtandao wa maeneo ya kutazamia mienendo ya majangiri hifadhini yanayokuwa na watu masaa ishirini na nne. Zaidi ya hayo, mtandao wa redio za kidijitali sambamba na kanzidata ya utekelezaji wa sheria uhakikisha kuwa rasilimali chache za Grumeti hutumika kikamilifu na kwa uhakika.

Skauti wa hifadhi

Grumeti Fund imeajiri timu ya skauti mia moja. Wote hutokea katika jamii za wenyeji wanaozunguka hifadhi yetu, na wengi wao wana historia ya kujihusisha na ujangiri. Skauti hupitia mafunzo endelevu kuendeleza viwango vya juu kwa ubora na usalama. Hii hujumuisha kufuata ratiba ya ukakamavu Madhubuti, mafunzo ya silaha, kozi za kujihami, mafunzo ya matibabu ya kuumia na misingi ya mawasiliano ya redio.

Soma zaidi
Scouts on the lookout at one of the Observation Posts (photo Roshni Lodhia)

Kikosi cha pamoja cha intelijensia

Kikosi cha pamoja cha Intelijensia ni ushirikiano kati ya Kitengo cha Utekelezaji wa sheria cha Grumeti Fund na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA). Kitengo hiki kidogo cha siri hutegemea mtandao wa watoataarifa kutoka vijiji na jamii za pembezoni nasi kupata taarifa za mienendo ya majangiri. Hii ni muhimu kwenye kuhakikisha kuwa kazi yetu ya uzuia-ujangiri ni ya kufahamu na kutekeleza kabla ya tukio kuliko kuitikia wakati wa tukio. Tunapambana kuweza kuwakamata majangiri wanaoingia hifadhini kuliko kukabiliana nao na kuwakamata baada ya wanyamapori kuwa wameshauriwa.

SPECIAL OPERATIONS

Kundi la operesheni maalumu

Ndani ya kikosi cha skauti wa hifadhi, kuna kikosi cha operesheni maalumu chenye skauti kumi na nane mahiri ambao wamethibitisha kuwa bora zaidi; skauti wenye uaminifu usionashaka na maadili ya kazi ya hali ya juu. Hupatiwa mafunzo endelevu ya kisasa na vifaa vya kiteknolojia, wakiwa wamepatiwa jukumu la kukabili usalama wa hali ya juu wa mapori ya akiba ya Grumeti. Wamewekwa kama kitengo cha kuitikia kwa haraka vitisho vya ujangiri pamoja na kulinda faru weusi walio hatarini kutoweka.

Teknolojia ya kibunifu

Idara ya kuzuia-ujangiri na utekelezaji wa sheria ya Grumeti Fund hutumia teknolojia mbalimbali za kibunifu. Hii hujumuisha mfumo wa ufahamu wa kikoa, kamera za TrailGuard, ndege zisizo kuwa na rubani, kikosi cha mbwa, vifaa vya kuona usiku pamoja na vifaa vingine bora kwa ajili ya mafunzo matumizi ya skauti.

Ndege zisizo na rubani

Ndege hizi zisizo kuwa na rubani hutumika kwa ajili ya uangalizi wa maeneo na zina uwezo wa kufanya kazi masaa ishirini na nne.

Vifaa vya uono usiku

Skauti mahiri wamepatiwa teknolojia bora ya kuona usiku, kuwawezesha kufanya kazi pasipo kugundulika gizani.

Mfumo wa ufahamu wa kikoa

Mfumo wa Ufahamu wa Kikoa ni zana ya teknolojia ya hali ya juu ambayo hutuwezesha kukusanya na kuunganisha taarifa kutoka idara mbalimbali.

TrailGuard

TrailGuard ni teknolojia mpya inayotumika Grumeti ikijumuisha mfululuzo wa kamera za siri iliyounganishwa na DAS.

Mafanikio

4x
Ongezeko la idadi ya tembo mara nne zaidi mbali na shida ya ujangiri afrika

100
Majangiri waliobadilika na kuwa watunzaji wa wanyamapori

7237
Waliokamatwa kwa shughuli za ujangiri na utumiaji haramu wa maliasili

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia