Kuhusu sisi

Grumeti Fund ni shirika lisilo la kutengeneza faida linalojishughulisha na kazi ya uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya jamii katika ukanda wa Ikolojia ya Magharibi mwa Serengeti nchini Tanzania.

Ndoto yetu ni kuwa na ulimwengu ambao binadamu na wanyamapori huishi pamoja kwa uendelevu, siku zote.

Hadi sasa, zaidi ya wafanyakazi mia moja sitini na tano hulinda, husimamia na kuangalia pori tengefu la Grumeti ambalo hapo awali yapata miaka 20 iliyopita halikuwa na wanyama,  na sasa limefurika wanyamapori tena. Ari na kujitoa kwao kunasukumwa na historia na kuongozwa na taswira pana.

Shabaha Yetu

Shabaha ya Grumeti Fund ni kushirikiana kuchangia kwenye uhifadhi wa Ikolojia ya Serengeti na kuinua jamii za wenyeji. Kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania na wadau wengine muhimu, tunahamasisha njia bora za uhifadhi na kushirikiana kimawazo kupunguza madhara.

Replacement Pic EEC_p7. _Option 2_ Tara Shupe

Historia Yetu.

Tunapatikana uwanda wa Magharibi mwa Ikolojia ya Serengeti, eneo linalotazamiwa na watu kuwa hazina ya kimataifa, maeneo ya Grumeti ni mazuri na yenye utajiri wa mimea na wanyama. Lakini hayakuwa hivi siku zote. Mwishoni na mwanzo wa karne, uwindaji haramu na ujangiri uliokithiri, ulipelekea kupungua kwa idadi ya wanyamapori na kusababisha umaskini kwenye jamii za pembezoni.

Kwa bahati nzuri, mwaka 2002, Mfadhili Mmarekani Paul Tudor Jones akaonesha nia binafsi ya kipekee ya kurejesha hali ya mapori haya katika ubora wake. Alianzisha Grumeti Fund na kuanza kurejesha eneo hili katika ubora wake wa awali. Baadaye waliungana na kampuni kubwa ya utalii duniani ya Singita.

Umoja huu wenye malengo, sambamba na usimamizi madhubuti na mbinu za utekelezaji wa sheria, umesaidia idadi ya wanyama kuongezeka kwa kasi, na kuifanya Grumeti kuwa kisa cha kipekee kwenye uhifadhi na moja kati ya maeneo pendwa ya utalii wa picha barani Afrika.

Tunapopatikana

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia