Washirika wetu

Grumeti Fund inathamini ushirika wa nje na kushirikishana mawazo. Kupitia kutengeneza fursa na wataalamu tunaongeza matokeo chanya. Kuanzia wadau wakubwa wa serikali hadi watengenezaji wa teknolojia ya uzuiaji-ujangiri na wataalamu wa kutengeneza biashara, tunajivunia kuzitambua taasisi na makampuni yafuatayo kama washirika wetu.

“Singita ni chapa ya uhifadhi ambayo imekuwa ikitunza nyika za Afrika kwa miaka 25 iliyopita, ikiwapatia wageni uzoefu wakipekee wa safari kwenye hoteli zake zilizoshinda tuzo kubwa ulimwenguni na kambi 12 za kifahari zilizoko sehemu tano tofauti barani Afrika. Kwa kushirikiana na mfuko usiowakutengeneza faida na asasi ambazo hutekeleza miradi ya uhifadhi katika kila eneo, Singita inatunza mazingira haya mazuri, kuchangia ongezeko la idadi ya wanyamapori, na kusaidia kuboresha uchumi wa jamii pembezoni mwa maeneo haya.

“Lengo la Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ni kuhifadhi na kutumia kwa uendelevu rasilimali za wanyamapori kwenye maeneo yaliyohifadhiwa. Kufanikisha hili, TAWA inashirikiana na jamii za wenyeji na wadau wengine wa kitaifa na kimataifa ili kizazi cha leo na kesho cha watanzania, na ulimwengu mzima wafaidike.”

 

“Lengo la Taasisi ya Uhifadhi na Jamii Afrika ni kuchangia kwenye utunzaji wa maliasili,na kuwezesha jamii sinazoishi pembezoni mwa maeneo haya, kuchangia kuwa na ulimwengu ambao watu na wanyamapori huishi pamoja kwa uendelevu, milele.”

 

“Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania huchangia kwa kiasi kikubwa kwenye kazi ambayo Grumeti Fund inafanya kutunza wanyamapori na kutekeleza miradi ya utafiti kama vile kuwavisha kola tembo.”

“Ni shirika lililoko Seattle na limeendelea kuwa mdau mkubwa wa Grumeti Fund. Kutumia teknolojia kuwezesha shughuli za uhifadhi hifadhini kumebadilisha siyo tu namna Grumeti Fund inavyofanya kazi bali namna uhifadhi unavyofanyika kote Afrika.”

“Grumeti Fund inashirikiana na wakuzaji wa biashara kutoka Afrika Kusini kutoa elimu ya biashara kwa wajasiriamali, kuwapatia jukwaa la kuhamasisha kujifunza, na uangalizi utakaopelekea mafanikio ya kibiashara.”

 

“Mnamo mwaka 2019 EWT iliongoza mafunzo mara mbili ya ukabilianaji na sumu kwa wadau wa Grumeti Fund, TAWA na TANAPA, kuwafundisha namna ya kutambua, kuitikia na kuzuia kuathiriwa na sumu kwa wanyamapori ndani ya Serengeti.”

 

“Mradi dada wa Grumeti Fund  huko Zimbabwe unashikilia na kushiriki maarifa yenye thamani kwenye uangalizi mzuri wa faru weusi pamoja na shughuli nyingine za wanyamapori, vyote vimekuwa muhimu kwa kazi iliyofanywa na Grumeti mwaka 2019.”

“Kuungana na Kijiji cha Lugha Concordia mwaka 2017 na kumeendelea kukuwa, kutoa elimu kwa wanafunzi wengi na walimu kila mwaka. Furaha, kujali na haiba ya timu ya Concordia huonekana. Programu hii, ya kwanza na ya pekee Tanzania, imetengeneza mabadiliko ya kudumu kupitia mtindo wa ufundishaji ambao huongeza uwezo wa lugha ya Kiingereza kwa wanafunzi, kuwaandaa kwa mafanikio katika shule za sekondari na kuendelea.”

“Jamii ya Wakufunzi wa Mbwa ya Kimarekani imekuwa ikitoa mafunzo kwa kitengo cha Mbwa Grumeti Fund tangu mwaka 2017. Wameiwezesha timu yetu kuwa waangalizi wa kiwango cha kimataifa hadi kuwa wakufunzi. Hii imewafanya kuwa miongoni mwa vitengo vya mbwa chenye uzoefu zaidi Afrika”

 

“Mwaka 2019, Grumeti Fund ilizindua ushirika mpya na programu ya chuo kikuu cha Stanford ya uhifadhi wa jenomu, wapokeaji wa uzinduzi wa urafiki wa utafiti wa Faru mweusi.  Kwa pamoja hufanya kazi kuelewa vema masuala mbali mbali kwenye mafanikio ya uhamishaji wa faru weusi wa mashariki – mada ya utafiti yenye tija kubwa kwenye jitihada endelevu za kuanzisha upya spishi hii kwenye maskani yao ya awali.”

“Kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, uhusiano kati ya Grumeti Fund na maabara ya Wittemyer ya CSU umekuwa sehemu muhimu kwenye mafanikio ya programu ya kuwawekea tembo kola, kwa ushauri wa CSU kwenye namna nzuri ya kufunga kola na aina ya somo, pamoja na ushirikiano kwenye tathmini mpya za mfumo wa tembo wanavyovamia mazao na tabia zao.”

 

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia