Kuwaandaa Mabingwa wa Uhifadhi

Kuna mithali ya Kiswahili isemayo “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”. Ni ukweli wa muda wote wenye uhalisia katika tamaduni nyingi, mabara na kazi – ikiwemo na uhifadhi.

Tunaamini kuwa kama tunataka baadaye ambayo watu wanaishi kwa amani na usawa na asili, lazima tuanze kwa kuwezesha kizazi kijacho leo. Ndio sababu tulizindua programu yetu ya Elimu ya Uhifadhi kwa watoto – mpango mahsusi uliyoundwa kupanda mbegu za upendo wa mazingira na wanyamapori kwa watoto wenye umri wa miaka 7 hadi 15.

Ndio tunafanya vikao vya uhamasishaji wa jamii na watu wazima, wanafunzi wa sekondari na wa vyuo vikuu – lakini mpango huu ni wa kipekee. Umeundwa mahsusi kwa watoto wa shule ya msingi, ukichanganya elimu na ubunifu kuwafundisha juu ya ikolojia, tabia za wanyamapori, na vitendo vya uhifadhi katika namna ambayo ni shirikishi, yenye ari na sahihi kulingana na umri wao.

Kupitia vipindi shirikishi na sanaa na ufundi wa asili tunakuza upendo wa kina na heshima kwa ulimwengu wa asili. Watoto sio hujifunza tu – wanashikamanishwa. Wanauliza maswali, huchafuka mikono na kuona jinsi chaguzi zao zinavyofaa. Na kwa kila kipindi tunapiga hatua moja karibu na kujenga kizazi cha wasimamizi wa mazingira ambao watabeba tochi hii mbele.

 

Mshikamano Unaotengeneza Mabadiliko

Lise Levy, Mshauri kutoka Wild Nature Institute, akishirikiana kwa karibu na waalimu wakati wa warsha.

Mwishoni mwa mwaka jana idara yetu ya RISE na Mahusiano kwa kushirikiana na Taasisi Wild Nature Institute – ambao wana zaidi ya muongo mmoja wa uzoefu kaskazini mwa Tanzania wakifanya mpango kama huu – na mpango wa elimu wa Tanzania waliongoza semina ya siku mbili ambayo ilileta pamoja walimu kutoka shule za msingi za zinazopakana na mapori yetu ya akiba.

Lengo? Kuwawezesha waalimu na zana, maarifa, na ujasiri wa kuongoza elimu ya uhifadhi katika vyumba vyao vya madarasa.

Matokeo yake? Makubwa. Shauku, kujitolea, na shauku kutoka kwa waalimu hawa ilikuwa zaidi ya kutia moyo. Waliondoka wakiwa wamewezeshwa na tayari kuwa mabingwa wa mabadiliko katika shule zao.

 

Kuleta mabadiliko – wiki moja, somo moja kwa wakati

Marykinoi Lembris, moja wa timu yetu akiongoza moja kati ya kipindi na Watoto.

Mwaka huu, timu yetu ilianza kufanya ziara za kila wiki na kuongoza vipindi kwa kila shule nane za kwanza zilizochaguliwa. Kila ziara inajumuisha kipindi cha saa moja kilichojaa hadithi, sayansi, ubunifu, na mazungumzo – yote iliyoundwa ili kufanya uhifadhi kuwa halisia, unaofaa na binafsi kwa wanafunzi hawa.

Kwa wastani wa wanafunzi 70 kwa kila darasa na madarasa saba katika kila shule, tunategemea kufikia zaidi ya wanafunzi 3000 mwaka huu kwenye shule hizi nane pekee yake. Hii humaanisha vijana 3000 kupata nyenzo na msukumo wa kutunza sayari yetu. Tunaamini pia katika kupima matokeo sio tu kutarajia. Wanafunzi wanajaza dodoso kabla ya programu kuanza na tena mwishoni mwa mwaka ili kufuatilia ukuaji katika uelewa wao wa uhifadhi na mazingira.

 

Kutazama Mbele

Wanafunzi wakiwa na furaha katika moja kati ya vipindi.

Tunapotazamia kupanua programu hii kufikia shule nyingi mwakani, tunakuwa na shauku kubwa. Tunajua kuwa mabadiliko hayatokei mara moja – lakini hutokea wakati akili za vijana zinawezeshwa kutunza, Kutenda, na kuongoza.

Kupitia elimu na ubunifu sio tu tunawafundisha watoto juu ya uhifadhi, bali tunatengeneza ubaadaye ambapo watu na asili hustawi pamoja.

Kwa sababu unapomfundisha mtoto kupenda dunia, sio tu unabadilisha maisha yao unabadilisha ulimwengu.

Unaweza kusaidia kufanya hivyo. Mchango wako unaunga mkono moja kwa moja juhudi zetu za elimu ya uhifadhi kwa kutoa vifaa, usafiri, na mafunzo kwa mashujaa wanaowafundisha.

Changia sasa na uwe sehemu ya kutengeneza kizazi kitakacho linda sayari yetu kwa miaka mingi ijayo.

 

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia