Kuziba Mwanya: Mawasiliano kama zana ya uhifadhi kuanzia kwenye jamii

Je! Ni faida gani ya utafiti wa msingi ikiwa hakuna mtu anayeweza kuielewa?

Katika uhifadhi ambapo uharaka hukutana na ugumu, uwezo wa kuwasilisha kwa ufasaha sayansi sio ustadi tu – ni jambo la lazima. Takwimu zinaweza kupelekea maamuzi lakini ni hadithi ambazo zinahamisha watu kuchukua hatua. Hii ndio sababu Kituo cha utafiti cha RISE Grumeti kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Leiden, hivi karibuni waliandaa na kuongoza warsha ya Hadithi/masimulizi ya Sayansi – hatua ya ujasiri kuelekea kuwezesha wanasayansi wa uhifadhi wa Tanzania kuwa na zana za kufanya kazi zao zisikike kweli kweli.

Kuanzia Aprili 28 hadi Mei 1 mwaka huu, wanasayansi kumi wa uhifadhi walikuja pamoja kuangazia jinsi utafiti wao unavyoweza kufanya zaidi ya kujaza majarida ya kitaaluma – zinaweza kuchochea mazungumzo, kuarifu sera, na kuongeza ushirikiano kwenye jamii. Kupitia mijadala, mafunzo kwa vitendo, kazi kwa vikundi na ushauri kutoka kwa wawezeshaji wenye uzoefu, washiriki walijikita kwenye kuelewa sanaa na sayansi ya hadithi: Kuunda simulizi zinazoweza kusikika, na kutengeneza taswira zenye kuvutia, na kuchuja tafiti ngumu kuwa jumbe nyepesi zenye kueleweka nje ya uwanda wa wanazuoni.

Hii haikuwa semina tu. Ilikuwa juu ya kubadilisha muelekeo.

“Kama wanasayansi, mara nyingi tunazungumza baina yetu,” alisema mwezeshaji wa semina na mtaftaji wa National Geographics Ghaamid Abdulbasat. “Lakini ikiwa tunataka mabadiliko – mabadiliko ya kweli ya kimfumo – lazima tuzungumze kwa njia ambazo umma unaweza kuelewa na kuungana nasi.”

Na unganisho ndio hasa semina hii ilihimiza.

Hadithi kwa ajili ya Sayansi inaendeshwa na dhamira ya kina: kutoa changamoto ni nani anayesimulia uhifadhi wa bara la Afrika. Mara nyingi masimulizi ya uhifadhi na wanyamapori wa Afrika yamekuwa yakisimuliwa na watu kutoka nje – na vyombo vya habari vya nje, NGOs za kimataifa au watafiti wa Magharibi. Masimulizi haya mara nyingi huwatenga watu ambao huingiliana na wanajua mazingira haya vema zaidi: jamii na wanasayansi wa Kiafrika.

Warsha hii inasaidia kugeuza huu utamaduni.

Ilizinduliwa mwaka 2022 na muikolojia na mwalimu Emily Strange ambaye alitumia tuzo yake ya kufundishia ya chuo kikuu kuunda mpango huu uliolenga Afrika Mashariki. “Tulitaka kutengeneza nafasi ambayo wahifadhi wa mazingira wanaweza kuibua changamoto kwenye masimulizi yaliyozoeleka. Nafasi ambayo wangeweza kuchunguza njia mpya za kuwasilisha kazi zao – njia ambazo ni za wazi, zenye uzito na zenye kuzingatia utamaduni.” Alisema Emily Strange

Kwa kuwalenga Watanzania, semina hiyo inawapa wanasayansi wa kitanzania kushiriki sio tu “nini” ya utafiti wao lakini “kwanini” – uhusiano, maadili na uzoefu wao ambao huchangia uhifadhi kwenye jamii.

Katika semina hii, washiriki walijifunza zana mbalimbali kama vile kurekodi sauti na picha hadi ArcGIS na namna ya kupanga mtiririko wa hadithi zitakazo wawezesha kushiriki kazi zao kwa njia za ubunifu na za kimkakati. Ujuzi huu ni muhimu kwa utetezi, elimu, ushiriki wa jamii na ushawishi wa sera. Mwisho wa semina hiyo kila mshiriki aliunda na kuwasilisha hadithi yake na kugeuza matokeo ya kisayansi kuwa hadithi za kidijitali zinazopatikana kwa wepesi ambazo zinaonyesha maarifa ya wenyeji, changamoto za haraka na mafanikio ya uhifadhi.

“Jamii za wenyeji ziko katikati ya juhudi zetu za utafiti na uhifadhi,” alisema Hillary Mrosso mtafiti kutoka Shirika la Utafiti na Uhifadhi la Tanzania (TRCO). “Kwa kujifunza jinsi ya kuwasilisha sayansi kwao itafanya kazi yetu iwe rahisi sana.”

Matokeo ya aina hii ya mafunzo ni makubwa. Wakati wanasayansi wa uhifadhi wanapokuwa wasimuliaji wazuri, kazi zao zinapatikana zaidi, zinakuwa na ushawishi zaidi na zenye athari zaidi. Watengenezaji wa sera huanza kusikiliza. Jamii zinaanza kujihusisha. Mabadiliko huanza kutokea.

Katika ulimwengu ambao mazingira ya asili yanaharibika na bioanuwai wako kwenye tishio la kutoweka; Hadithi inaweza kuwa moja ya zana muhimu zaidi tulizonazo.

Asante kwa kujitolea kwa timu yetu, wawezeshaji na wanasayansi ambao walijiunga nasi katika safari hii, hadithi ya uhifadhi wa Tanzania inasimuliwa – wazi zaidi, kwa ujasiri na kwa sauti za wale wanaoiishi kila siku.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia