Stanslaus Mwampeta

Mkuu wa Utafiti na Ufuatiliaji (Muikolojia)

Akiwa na umri wa miaka saba tu, baba yake Stanslaus alimwezesha kugundua maajabu ya Serengeti. Uzoefu huu wa mapema katika umri mdogo uliwasha cheche ndani yake, na kuamsha shauku yake ya muda mrefu ya kupenda mazingira ya asili. Miaka miwili ya kumbukumbu hizo muhimu huko Mugumu, mji mdogo karibu na Serengeti, na safari chache katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, vilikuza shauku yake ya uhifadhi.

Kwa shauku kubwa na mazingira ya asili, Stan alifanya masomo yake kwa malengo. Alipata BSc. Ya Sayansi ya Wanyamapori na Uhifadhi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Akiendelea na safari yake ya kimasomo katika taasisi hiyo hiyo, alifanya tasnifu ya uzamili iliyohusu ikolojia ya caracal na serval. Sanjari na hayo, Stan alifuatilia shughuli za makundi ya simba katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Uzoefu huu ulifungua njia kwa utafiti wake wa udaktari. Katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Norway, alijikita kufanya Ph.D. yake kuboresha mbinu za makadirio ya idadi ya simba. Michango yake ya kitaaluma imechapishwa katika majarida makubwa mbalimbali.

Kwa zaidi ya muongo mmoja Stan amekuwa akifanya kazi Serengeti, na kuweza kupata kujua siri zake ndani na nje. Hadi kufikia wakati alipojiunga na Grumeti Fund mnamo mwaka 2023, maarifa yake yalikuwa ya kifani. Kama mkuu wa Utafiti na Ufuatiliaji, anaongoza timu iliyojitolea yenye dhamira moja: kukusanya na kutafsiri data za ikolojia ili kulinda afya na ustawi wa mfumo wa ikolojia.

Stanslaus alijifunza umuhimu wa ushirikiano kwenye uwanja wa mpira, na sasa analeta ari hii katika mfumo wa Ikolojia wa Serengeti Magharibi. Anaamini kuwa uhifadhi unavuka sayansi–ni juhudi za pamoja. Akiwaalika washiriki wa ndani hadi wataalamu wa kimataifa, humuita kila mtu uwanjani kushiriki maarifa na nyenzo kama vile pasi katika mechi ya kusisimua. Lengo lake? Ni kuwa na sayari inayostawi kwa watu wote.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia