Matty Perry

Meneja Mkuu – Uzuiaji-Ujangiri & Uhifadhi

Matt amefanya kazi kwenye sekta ya uhifadhi kwa muda zaidi ya miaka 18. Aliungana na Grumeti Fund kama meneja wa kanda mwaka 2008 na aliendelea kukuwa hadi kupandishwa cheo na kuwa meneja wa uhifadhi mwaka 2016. Hivi karibuni, Matt aliteuliwa kuwa Meneja Mkuu ilikusaidia kuongoza Grumeti Fund. Ni meneja mzoefu mwenye stadi kwenye uhifadhi, utekelezaji wa sheria, na kupanga na kutekeleza mikakati ya uhifadhi na uongozi. Kuanza kwake kazi kwenye hifadhi maarufu ya taifa ya Kruger kulimpatia Matt msingi dhabiti na uelewa wa changamoto ngumu za usimamizi zinazokabili maeneo yanayohifadhiwa Afrika. Kutokea Kruger, Matt aliendelea kushauri miradi mbalimbali nchini Zimbabwe, Namibia na Tanzania.

Kwa miaka, Matt ameweza kujikita binafsi kwenye shughuli za kuingia hifadhini na masuala ya utekelezaji wa sheria wa mradi huu wa kipekee wa uhifadhi, jambo lililomfanya aweze kuzungumza Kiswahili kwa ufasaha. Kuwa sehemu  ya mradi huu wa uhifadhi kumekuwa na faida kubwa kwa Matt na amekuwa akifurahia kufanya kazi na timu mbalimbali za watu wenye ari kwa miaka yake ya uzoefu wakihifadhi, katika maeneo haya mazuri ya hifadhi ulimwenguni. Matt ametumikia Grumeti Fund kwa zaidi ya muongo sasa, na anajivunia mafanikio yaliyopatikana, pia, amejizatiti kuhakikisha kuwa kisa hiki cha kipekee kinaendelea kuwa na faida kwa watu na wanyamapori wa Serengeti.

Matt amekulia Kwa-Zulu Natal, Afrika Kusini. Kutokana na upendo wake wa uhifadhi alisoma diploma ya uhifadhi wa asili kutoka chuo cha teknolojia cha Tshwane nchi Afrika Kusini. Mwaka 2017, Matt alimaliza Shahada ya uzamili ya uongozi wa uhifadhi katika chuo kikuu cha Cambridge.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia