Noel Mbise

Meneja Mkuu – Utafiti & Jamii

Noel alijiunga na Grumeti Fund mwaka 2015. Kabla ya hapa alikuwa muikolojia wa Hifadhi za Taifa za Tanzania (TANAPA)katika usimamiaji wa maliasili na uhifadhi kwa muda wa miaka sita.  Katika umri wake mdogo, Noel amefanya kazi katika sekta ya utalii  na taasisi za fedha. Stadi zake ubobezi ni kwenye usimamiaji wa mazingira na ikolojia ya nchi kavu, uchambuzi wa sera, na uundaji na utathimini wa miradi ya uhifadhi. Pia ni mtaalamu kwenye uendelevu wa biashara, uchambuzi wa madhara ya kimazingira na kijamii, ushauri wa kimazingira, na uvumbuzi wa kiteknolojia kwa tafiti za uhifadhi na usimamizi.

Noel amekulia kusini-mashariki mwa mlima Meru, Tanzania. Mandhari za msitu, sauti na harufu vilikua sehemu kubwa ya utoto wake. Kukulia katika mazingira haya ya asili kulisukuma hamu yake ya uhifadhi. Mwaka 2014 Noel alipata Shahada yake ya uzamivu ya Sera za Kimataifa za Mazingira  kutoka Monterey Institute of International Studies California ambapo alijikita kwenye Uongozi wa Maliasili/ Sera na Uendelevu wa Mazingira. Mwaka 2019 Noel alipata MBA yake kutoka African Leadership Academy Faculty of Business. Kabla ya masomo yake ya juu, Noel alipata shahada ya sayansi katika usimamiaji wa wanyama pori kutoka chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine Morogoro, Tanzania.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia