Frida Mollel

Meneja wa Idara ya Ufikiaji wa jamii

Frida alijiunga na Grumeti Fund mwaka 2010. Kabla ya kuja Serengeti, amekuwa mwalimu wa sekondari kwa muda wa miaka tisa, akifundisha masomo ya Kemia na Bayolojia. Miongoni mwa uzoefu wake ni pamoja na kuwa Mkuu wa Mafunzo na Uhamasishaji wa Jamii (TRACE) kwa miaka mitatu kwenye kituo cha Umoja Cha Sweden – Vi Programu ya Kilimomsitu Musoma na miaka miwili kama Afisa Mkuu wa Programu yenye kuhusisha kutatua changamoto mbalimbali za jamii, utekelezaji wa njia na miradi ya uhifadhi endelevu wa bayonuai na kuboresha maisha ya jamii.

Frida amekuwa akijikita kwenye shughuli za usimamiaji wa maliasili, hasa usimamiaji wa misitu, usimamiaji wanyamapori, tathmini ya madhara ya kimazingira, uwezeshaji wa mafunzo kwenye masuala ya uhifadhi wa asili na miradi yenye matokeo chanya kwenye mazingira.

Wakati wa ukuaji wa Frida huko Arusha, Arusha ilikuwa ikijulikana kama “Geneva ya Afrika”, kutokana na hali yake ya hewa nzuri, mvua nyingi na aina nyingi za mimea na wanyama wenyekuvutia. Mazingira haya yenye kuvutia yalimhamasisha kuelekea kwenye uhifadhi na kusaidia kutunza mazingira mazuri ya asili ya nchi yake.

Frida ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo Kikuu Kilimo cha Sokoine, Morogoro, Tanzania. Mwaka 2021 alipata MBA yake kutoka African Leadership University School of Business, Kigali Rwanda. Michango yake ya kipekee katika uhifadhi ilimwezesha kutambuliwa kama mmoja wa Viongozi wanane mashuhuri wa Uhifadhi katika Bara la Afrika na alipewa udhamini kamili wa kushiriki katika programu ya MBA.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia