Progaramu ya Uhisani ya RISE: Kumwangazia Juma Minya

Mwaka 2019, Grumeti Fund ilianzisha programu yetu ya Utafiti na Ubunifu kwa ajili ya Mfumo wa Ikolojia ya Serengeti (RISE). Programu za RISE huvuka mipaka ya utafiti wa kawaida. Kwa kutumia vipaji na wasomi wenye maono Tanzania na nje ya nchi, RISE inajenga daraja kati ya utafiti wa kiwango cha juu wa kisayansi na maamuzi ya uhifadhi yanayotekelezeka. Kituo cha RISE daima hufurikwa na wasomi wapya na wanasayansi wenye uzoefu ambao kwa pamoja wanashughulikia maswali muhimu katika sayansi ya uhifadhi na kutafuta suluhu zinazowanufaisha wanyamapori na jamii zinazotegemea mfumo wa Serengeti.

Juma Minya ni miongoni mwa wanasayansi ambao wanafanya kazi ya kusukuma gurudumu la sayansi ya uhifadhi mbele kupitia RISE. Juma anafanya Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Uhifadhi kutoka Chuo Kikuu cha Glasgow. Mwaka 2022, RISE ilimpatia uhisani wa masomo yake na kufanya utafiti kwenye mapori ya akiba ya Grumeti kuhusu takwimu za tembo. Hasa, Juma ana nia ya kuelewa miundo ya umri na jinsia ya tembo katika mfumo huu wa ikolojia, ambayo anaamini itatusaidia kuelewa sababu zinazochangia migogoro kati ya binadamu na tembo.

Akirejea alivyopata uhisani wa RISE, Juma alielezea, ” niliona tangazo la uhisani kwenye tovuti ya Grumeti Fund mwezi wa tatu mwaka 2021. Nikiwa nimejaa matumaini na azimio, nilituma maombi yangu, na nilipewa nafasi ya kuanza masomo yangu mwaka 2022. Kwangu hii ilikuwa nafasi ya kipekee na adhimu.”

Juma anahusisha shauku yake ya sasa kwa wanyamapori na kukulia pembezoni mwa mfumo wa Ikolojia ya Serengeti-Mara Mkoani Mara, Tanzania. Anakumbuka kuwaona nyumbu na wanyama wengine wakivuka Mto Mara wakati wa uhamaji wao mkubwa kila mwaka. Akikumbuka matukio hayo, alisema, “bado nakumbuka kuwaona wanyama pori wakivuka mto na kutembea kwenye mazingira yao ya asili kutoka nyumbani kwetu. Uzoefu huu wa kustaajabisha na wenye kudumu uliibua shauku yangu ya kuwalinda na kuwatunza wanyamapori.” Hamasa binafsi ya Juma kwa wanyamapori ilimuongoza kwenye safari yake ya masomo; mwaka 2014, alihitimu Shahada ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, na kuweka msingi wa mustakabali wake wa baadaye katika sayansi ya uhifadhi.

Hamasa ya Juma kufanya utafiti wake iliibuliwa na malalamiko ya jamii kuhusu migogoro ya binadamu na wanyamapori. Akilizungumza hili, Juma anaeleza, “Kila mwaka, idadi ya tembo inaongezeka nchini Tanzania, na kupelekea migogoro kati ya binadamu na wanyamapori. Kugundua chanzo kikuu cha mienendo ya tembo katika jamii zinazopakana na eneo lililohifadhiwa ni hatua moja wapo kuelekea suluhisho endelevu.”

Mwezi Mei 2023, Juma alianza kukusanya taarifa za awali za utafiti wake kwa kushirikiana na timu ya RISE; pamoja, walizunguka maeneo mbalimbali ya mapori ya akiba ya Ikorongo – Grumeti na eneo la Usimamizi wa Wanyamapori la Ikona (WMA), wakitambua makundi ya tembo na idadi ya yao. Juma anatarajia kukamilisha hatua ya kukusanya data ya utafiti wake mwezi Agosti 2023.

Akizungumzia matokeo ya utafiti wake, Juma alisisitiza jinsi vigezo vya umri na jinsia vinavyochangia ukuaji wa idadi ya tembo na mienendo yao. Akitoa mfano wa jinsi utafiti wake unavyoweza kutumika, alieleza, “kundi la tembo lenye watoto wengi lina uwezekano mdogo wa kwenda kwenye maeneo ya jamii za pembezoni kwa sababu tembo wakubwa majike ambao ni viongozi wa kundi hufanya mahamuzi sahihi kati ya kuishi na kufa kutokana na kumbukumbu zao za muda mrefu zinazowawezesha kukumbuka matukio ya zamani yanayohusiana na hatari na upatikanaji wa rasilimali. Kuelewa vigezo vya umri na jinsia kutatuwezesha kuelewa hali ya sasa na kutabiri matukio ya baadaye.”

Juma anatumaini kazi kama yake itawachochea kufikia ubadaye ambao wanyamapori na jamii wataishi pamoja bila migogoro. Alieleza, “Natumai kuona jamii ambapo binadamu na wanyamapori wanakaa kwa pamoja kwa amani siku zote; hili ndio lengo kuu la utafiti huu – kupata suluhisho bora zitokanazo na mtazamo wa jamii za pembezoni mwa hifadhi ambazo zitapelekea kuishi kwao kwa amani na wanyamapori.”

RISE inalenga kuendeleza vipaji vya ndani na kuwawezesha watu wanojituma, kama Juma, ambao wana ari na shauku kubwa ya kulinda maeneo yaliyohifadhiwa na rasilimali za asili za Tanzania. Kupitia programu ya uhisani, RISE hutoa fursa kwa wapenda uhifadhi Tanzania nzima; kwa sasa, Juma ni miongoni mwa wasomi wanne wanapata uhisani wa masomo yao ya shahada ya Uzamili au Shahada ya Uzamivu katika fani zinazohusiana na uhifadhi. Programu hii ni sehemu tu ya jumla ya njozi ya RISE ya kutengeneza zana, suluhisho, na uwezo ambao utakabiliana na matatizo ya uhifadhi yanayohitaji hatua za dharura na kusaidia maamuzi endelevu kwa watu na wanyamapori.

Kuwa sehemu ya njozi yetu leo. Kuchangia, bofya hapa.

 

 

 

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia