Kuwawezesha Walinzi wa Wanyamapori

Askari wetu waliojitolea kupambana na ujangili walipitia programu ya kuboresha ujuzi wao mwezi Januari. Chini ya uelekezi wa Simon Leaks kutoka Big 5 Protection, mafunzo haya maalum ya ujuzi wa kufuatilia yalilenga kuinua uwezo wao wa kulinda wanyamapori kwa viwango vya juu.

Simon alisisitiza jukumu muhimu la ujuzi wa kufuatilia, akisema, “Kila skauti anahitaji kuwa mfuatiliaji mzuri. Hatima ya faru, tembo, na wanyamapori wengi hutegemea ujuzi huu.” Glen Steyn meneja wetu wa kupambana na ujangili alielezea furaha yake kuhusu mafunzo hayo akiona kuwa ni mwanzo tu wa mpango wa kina. Ifikapo mwisho wa mwaka lengo ni skauti wote themanini kuwa na ujuzi huu muhimu, kuwageuza maskauti kumi wa kwanza kuwa mabalozi wa maarifa ambao watashiriki utaalamu wao na timu nzima.

Timu yetu ya kupambana na ujangili inayojumuisha maskauti themanini, askari sitini na wanne katika Vituo vya Uangalizi (OPs), vitengo vya doria vinavyohamishika, na Kikundi Maalum cha Operesheni (SOG), ina jukumu muhimu katika ulinzi wa wanyamapori. Madhumuni ya msingi ya kozi hii ya ufuatiliaji ni kuwawezesha skauti na utaalam wa kufuatilia nyayo za wanyama pori na wawindaji haramu ndani ya mapori ya akiba ya Ikorongo – Grumeti, kuwawezesha kimkakati kukusanya taarifa muhimu kuhusu shughuli za ujangili.

Ingawa skauti wetu tayari wana ujuzi wa kimsingi wa kufuatilia, lengo lilikuwa kuwainua hadi ngazi ya juu. Amos Kisako mmoja wa maskauti kumi waliomaliza kozi ya siku ishirini na moja alishiriki ujuzi wake mpya, akisema, “Sasa ninaweza kufuatilia kundi la zaidi ya wawindaji haramu wawili kubaini idadi yao uzito na jinsia.”

Katika harakati zetu za kuhifadhi bila kuchoka, skauti wetu  wa uhifadhi hufanya kazi 24/7 na kufanya ujuzi huu wa juu wa ufuatiliaji kuwa muhimu sana. Ikiwa ungependa kuchangia shughuli zetu za kupambana na ujangili na kusaidia uhifadhi wa wanyamapori tafadhali bofya hapa. Kwa pamoja tuungane kuwalinda wakaaji wa thamani wa sayari yetu.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia