Kustawi Zaidi ya Biashara na Programu ya RED ya Grumeti Fund

“Nilikuwa nikifikiri elimu hukoma baada ya shule, lakini sasa nafahamu ni safari ya maisha yote” analisema akiwa na shauku ya hekima mpya. Hata wazee kama sisi wanaweza kuendelea kujifunza na kukua. Mpango huu uliniongeza ubunifu na ujuzi wangu wa kufikiri – ni zaidi ya biashara tu. Nilijifunza kujenga mahusiano imara na kuzitazama changamoto kama fursa. Imenipa njia mpya kabisa ya kustawi, sio tu katika biashara, bali katika maisha!”

Joyce Mazira, mama shupavu wa watoto watano, mkulima, na mjasiriamali kutoka kijiji cha Mihale alianza safari yake ya kuleta mabadiliko na programu yetu ya RED mwaka 2018.

Mabadiliko ya Joyce ni ushahidi wa programu ya Ustawishaji wa Biashara Vijijini (RED) ya Grumeti Fund. Tangu kuanzishwa kwake, mpango huu umekuwa zaidi ya ushiriki, umeweza kuwawezesha kikamilifu zaidi ya wakazi 1000 ili kuinua ujuzi wao wa ujasiriamali. Imekuwa safari yenye ukuaji, kupitia mbinu za utengenezaji wa bidhaa, kutambua fursa ambazo hazijatumiwa, na kufahamu usimamizi na upangaji wa fedha. Shauku inaendelea kuongezeka huku zaidi ya wanachama wapya 130 wakijiandaa kuanza safari yao ya mpango wa RED mwaka huu.

Joyce na Philip wakiwa katika kipindi, wakati Philip alipomtembelea nyumbani ili kutoa ushauri na usaidizi.

Anayeongoza mawazo haya mapya ni Philip, Afisa wa Programu ya Ustawishaji wa Biashara Vijijini (RED) ya Grumeti Fund, mshauri mwenye rekodi ya mafanikio. Akitafakari kuhusu safari yake, Joyce alisema, “Kabla ya RED sikujua jinsi ya kuweka akiba, kufuatilia mauzo yangu au kudhibiti faida yangu. Sasa, nashukuru kwa programu hii na usaidizi wa Philip, ninaendesha fedha zangu kwa ujasiri.

Ili kuwa sehemu ya safari hii ya mabadiliko bofya hapa na uchangie katika mpango wa RED. Jiunge nasi katika kukuza mabadiliko ya kudumu na kuwawezesha watu kustawi zaidi ya mipaka ya biashara—katika maisha yenyewe.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia