Kufungua Fursa: Davis Merinyo’s na Mafunzo ya Vitendo kazini Grumeti Fund

Programu ya Mafunzo kazini ya Grumeti Fund inatoa fursa kwa wanafunzi na wahitimu wa vyuo vikuu kupata uzoefu na kukuza stadi zao za kitaalamu katika fani zao. Davis Merinyo ni miongoni mwa wanafunzi waliopata nafasi kwenye programu hii ambaye ameleta mchango mkubwa wakati akishirikiana na Idara ya Mahusiano ya Grumeti Fund. Davis aliungana na Grumeti Fund miezi michache iliyopita baada ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine akiwa na shahada ya usimamizi wa wanyamapori. Tayari uzoefu wake kama mwanafunzi wa mazoezi kazini umekuwa na mchago katika maisha yake, ukibadilisha mwelekeo wake wa kazi na kusaidia maendeleo yake binafsi.

Davis amekuwa akifanya kazi kwa karibu na kitengo cha kuzuia migogoro kati ya binadamu na wanyamapori cha Grumeti Fund kilichopo Hunyari. Kitengo hiki husaidia kwenye matukio ya migogoro kati ya binadamu na wanyamapori katika jamii za pembezoni mwa mapori ya akiba ya Ikorongo – Grumeti. Akizungumzia siku yake ya kwanza, Davis anakumbuka vizuri ilivyokuwa, “Nilifika kwenye kitengo hicho saa nne usiku, na timu mara moja iliniomba nibadilishe nguo na kuwa tayari kwa simu zitakazo pigwa kuhusiana na matukio ya wanyamapori kutoka kwenye jamii. Nilishangazwa kuona timu inafanya kazi hata usiku.

Davis alieleza kwamba kufanya kazi kama mwanafunzi wa mafunzo kazini na Grumeti Fund kumempatia uzoefu wa vitendo ambao umemsaidia kuona uhusiano kati ya masomo yake ya awali chuoni na uhalisia. Kulingana na Davis, ameweza kujifunza zaidi akiwa kazini kuliko angevoweza kujivunza darasani. Mafunzo haya yamemsaidia Davis kuelewa njia mpya za kuzuia Migogoro kati ya binadamu na wanyamapori, kama kutumia mafataki na vilipuzi kuwazuia tembo; mafunzo haya yamempatia mtazamo mpya juu ya umuhimu kushirikisha jamii katika shughuli za uhifadhi. Kwa maneno yake mwenyewe, alisema, “Nimetambua kuwa uhifadhi unajumuisha si tu wanyamapori bali pia ustawi wa jamii zinazoishi pembezoni na maeneo yanayohifadhiwa.”

Ngoma za asili katika miongoni mwa vipindi vya elimu ya uhifadhi

Akizungumzia kuhusu kazi ambayo Grumeti Fund inafanya katika jamii za pembezoni na majukumu yake aliyokuwa nayo, Davis alieleza, “Kujitolea kwa Grumeti Fund katika kuinua jamii za eneo hili ni wa kipekee. Kushirikiana na kusikilizana kwa makini na watu wengine kulionekana kuwa njia yenye ufanisi zaidi ya kutambua mahitaji yao na kutatua masuala yao. Kushuhudia dhamira ya shirika katika kulinda maliasili kumenihamasisha. Kila kikao, nilishuhudia nguvu ibadilishayo ya elimu, ushirikishwaji wa jamii, na hamu ya kulinda na kuhifadhi wanyamapori.”

Stadi hizi zimemfungua Davis macho kuhusu tamaduni zinazojitokeza nchini Tanzania. Akizungumza kuhusu uzoefu wake, Davis alisema kuwa wakati kuwa na idara ya Mahusiano ya Grumeti Fund kumemwezesha kujifunza tamaduni na desturi mbalimbali tofauti na zake. Alifurahishwa sana na kujaribu vyakula vya Ladha mbalimbali kwenye jamii alizofanya kazi nao kwa karibu.

Davis wa kwanza kushoto, akipata maelezo namna tai za kuwafunga tembo shingoni zinavyotumika kutatua migogoro baina ya wanyamapori na tembo.
Programu ya mafunzo kazini ya Grumeti Fund inatoa uzoefu wa moja kwa moja, uangalizi, na fursa ya kuleta mchango chanya kwenye sekta. Programu yetu ya mafunzo inachangia kuendeleza kizazi kijacho cha wahifadhi wa mazingira na maliasili, lakini hatuwezi kufanya hivyo pekee yetu. Jiunge nasi leo katika misheni yetu. Kutoa mchango, bonyeza hapa.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia