Kuangazia programu ya wanawake kwenye uhifadhi

Grumeti Fund imejizatiti katika kuandaa viongozi shupavu wanawake kwenye sekta ya uhifadhi kwa vizazi vijavyo. Kwa kupitia programu yake ya wanawake kwenye uhifadhi (Women in the Field), Grumeti Fund imechangia kujenga uwezo na uzoefu kwa zaidi ya wanawake 28 tangu mwaka 2019. Programu hii ya wanawake kwenye uhifadhi ilianziswa mwaka 2019 ikiwa na washiriki wanne tu, na tangu wakati huo imekua na kufikia kiwango cha kupokea kati ya washiriki kumi na mbili hadi kumi na sita  kwa awamu mbili kila mwaka.

Programu hii hutoa mafunzo kwa vitendo kwenye masuala ya ikolojia na njia za tafiti za kijamii, njia za kuchakata taarifa na zana za kukua kitaaluma na kikazi. Baada ya mafunzo ya wiki tatu, washiriki huondoka wakiwa na stadi na uzoefu utakaowawezesha kuwa na mchango mkubwa kwenye uhifadhi. Vilevile washiriki huondoka wakiwa wametengeneza mtandao wa wanawake wenzao walioko kwenye sekta ya uhifadhi na utafiti.

Washiriki wengi wa WIF wataweza kufanya tafiti muhimu kwenye nyanja zao, na baadhi wameishaanza kuonesha mchango wao. Wawili miongoni mwa washiriki hao ni Vainess Lazier na Lucia Romward. Vainess ni miongoni mwa washiriki wa awamu ya kwanza ya WIF ambao walimaliza mafunzo yao mwaka 2019, na Lucia alishiriki moja kati ya vipindi vya WIF vya mwaka 2021.

Mwaka 2021, Vainess alirejea kituo cha RISE Grumeti Fund ili kuweza kuelewa vema tabia za kuzaliana za tai mwenye mgongo mweupe (White-Backed Vulture) kwenye mapori ya akiba ya Ikorongo – Grumeti.  Ametumia miaka miwili iliyopita kutafiti spishi hii muhimu – akiangazia tabia zinazoathiri kujenga viota, tabia zao za asili, na kukua kwa makinda wao katika eneo hili. Tafiti ya Vai itasaidia kufahamu vitisho vya kupungua kwa idadi ya hawa tai, ambayo itasaidia ufanyaji wa maamuzi ya kihifadhi hususani kuilinda hii spishi na ubora wa maskani yao.

Kiota cha tai kinafanyiwa utafiti kwa kutumia aplikesheni ya GoPro na na fimbo ya telescope.

Kuangazia wanawake kwenye uhifadhi: Vainess (Vai) Laizer

Vainess alikuwa miongoni mwa washiriki wa awamu ya kwanza ya WIF. Wakati huo, Vainess alikuwa akifanya mafunzo ya waongoza utalii, lakini alikuwa akitazamia kuegemea kwenye kazi za uhifadhi na tafiti; kwa programu hii kuwa ya wanawake pekee, aliona WIF ni mafunzo aliyohitaji ili kuweza kupenyeza kwenye sekta ya wanyamapori iliyotawaliwa na wanaume.

Alipoulizwa namna WIF imechangia kwenye tafiti yake ya sasa, Vainess alisema, “WIF ilifungua macho yake.” Vai aliisifia programu ya WIF kwa kumpatia ujasiri wa kufanya tafiti na kazi za uhifadhi. WIF ilimkutanisha Vai na washauri na watafiti wanawake wenyekutia moyo – akiwemo mwanasayansi mkuu wa RISE, Kristen Denninger Snyder – aliyeonesha mchango mkubwa wa wanawake kwenye utafiti na uhifadhi. Vai anasema, wanawake aliokutana nao wamemsaidia kutambua kuwa anaweza kutimiza ndoto zake.

“Grumeti Fund na RISE zimekuwa mbaraka kwenye maisha yangu kwa sababu wamenipatia jukwaa la kuonesha uwezo wangu na kufanya kile ninachopenda kufanya.”

– Vainess Laizer

Vai alimaliza mafunzo ya WIF akijihisi mwenye kuwezeshwa kutafuta watu wenye malengo na makusudi kama yake. Akiwa mwenye ujasiri katika stadi zake, uwezo wake, na ndoto zake, Vai ameweza kukabili changamoto za kuwa mwanamke aongozae timu ya tafiti. Alisema kuwa WIF imemuonesha umuhimu wa ushirikiano katika kukabili changamoto na ugumu katika uwanja wa tafiti.

Vai akirekodi taarifa za tafiti kwenye kiota cha tai wakati akiongoza timu ya ytafiti. Anahamisha picha na picha mnato za kiota kwenye simu yake kupitia kamera ya GoPro ambayo imeshikizwa kwenye telescoping rod.

Akizungumzia kuhusu kuelekea kwenye uwanja wa tafiti, Vai alisema: “sio jambo rahisi kuwa mwanamke katika uwanja huu.., lakini inawezekana – sio jambo ambalo wanaweza wanaume pekee yao, bali hata wanawake wanaweza, kama ukiwa na nia.”

Akizungumzia uzoefu wake kufanya kazi na Lucia, mshiriki mwenzake wa WIF, Vainess alisema, wakati akijisikia msukumo mkubwa kuwa mfano mzuri kwa Lucia, ameona zoezi lote kuwa ni uzoefu mzuri na wenye kustahili – “[wote kutokea katika programu ya WIF], tuko kama watoto wa mama mmoja.” Vainess anamshukuru Dr. Kristen Snyder kwa kuanzisha na kutengeneza kituo cha RISE. Kwa maneno yake, Vainess anasema, “RISE huwapatia watu wengi fursa ya kuhamasishwa.”

Ushauri wa Vai kwa wanawake wengine wanaotaka kujihusisha na uhifadhi:

“Fuata kile ukipendacho…ndoto zako ni muhimu…zungukwa na mazingira yanayokusaidia kukuwa.Sukumwa kuwa mkweli kwako na fanya jambo sahihi”

Vai anategemea kuona uhifadhi, tafiti, na ufanywaji wa maamuzi kuwa jumuishi huko mbeleni. Pia, anatamani kuona taasisi nyingi zikifadhili tafiti mbalimbali za kibunifu ambazo ni muhimu kwenye kufanya maamuzi.

Vainess ni mhitimu wa shahada ya utalii wa wanyamapori katika chuo cha African Wildlife Management University, mwaka 2017. Kwa sasa ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha kilimo Sokoine, na anatarajia kuhitimu mwaka huu. Pia, Vaines anatazamia kufanya masomo yake ya shahada ya uzamivu mbeleni. Vainess anapenda kuwa mtafiti mkubwa wa tai (na hatuna shaka atafanikisha hilo!).

Kuangazia wanawake kwenye uhifadhi: Lucia Romward

Lucia aliungana na Vainess mwaka 2022 kama mwanafunzi na msaidizi wa tafiti, na amekuwa akiambatana na Vainess porini kufanya tafiti za viota na ofisini akichambua taarifa. Lucia alifahamiana na Vainess kupitia mtandao wa WIF ambao ulitambua kuwa yeye na Vainess walikuwa wana shauku ya kufanana kuhusu tai.

Lucia (kushoto) akicheka wakati akiwa porini.

Programu ya WIF ilimvutia Lucia ambae kwa muda mrefu amekuwa akihamasishwa na wanawake wengine kwenye sekta ya uhifadhi, hasa wale wanaoleta chachu kwenye uhifadhi sambamba na kutekeleza majukumu ya kila siku kwenye familia. Kwenye mahojiano yake, Lucia aliwataja wanawake maarufu kwenye uhifadhi, kama vile Jane Goodall, amekuwa akimhamasisha binafsi kama mwanamke kwenye sekta ya uhifadhi.  Lucia alikuja kwenye programu ya WIF akiwa na ari ya kushirikiana na wanawake wengine wanaopenda kuleta matokeo chanya kwenye uhifadhi na tafiti.

Alipoulizwa namna WIF inaweza kukuza taaluma yake mbeleni, Lucia alisema kuwa programu ya WIF imemuwezesha kupata stadi mbalimbali na kumpatia uangalizi ambao umemfanya kuwa mtafiti mzuri. Aliongezea kwa kusema, kufanya kazi na wanawake wengine kumemsaidia kuongeza ujasiri, ambao utamsaidia kukabili changamoto mbalimbali kwenye uhifadhi.

Lucia anaamini wanawake wengi wanapatiwa fursa za kufanya kazi kwenye uhifadhi na tafiti. Anasema: “Nafikiri tunapiga hatua. Nategemea kuona wanawake wengi wakifanya kazi katika uhifadhi [mbeleni] kuliko hivi leo.” Wanawake wameunganishwa na mazingira kwa namna ya pekee, na kwa kiasi kikubwa, ubaadae wa uhifadhi na ulinzi wa mazingira huwategemea kwa kiwango kikubwa.

Alipoulizwa kwanini ni muhimu kuwahusisha wanawake kwenye uhifadhi, Lucia alisema, wanawake wanachangamana na mazingira kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania; aliongeza pia, ni kwa sababu wanawake mara nyingi huwa na wajibu wa kuwalea watoto, wanawake wenye uelewa na kuhusiana na uhifadhi watasaidia kutengeneza kizazi cha Watanzania chenye kutambua mazingira ya asili na uhifadhi.

Ushauri wa Lucia kwa wanawake wengine wanaotaka kujihusisha na kazi za uhifadhi:

 “Chochote awezacho kufanya mwanaume, mwanamke anaweza pia..jifunze kukabili changamoto kwa ujasiri….tafuta washauri wazuri [wanao kuunga mkono na kuambatana nawe].”

Miongoni mwa mada nyingi alizojifunza Lucia alipokuwa kwenye programu ya WIF, alivutiwa sana na mada zilizohusu ufanyaji wa tafiti za kijamii na kujumuisha jamii katika shughuli za uhifadhi. Anaelezea: “unapozungumzia uhifadhi hauwezi kuiondoa jamii kwa sababu mambo mengi hutegemea hizi jamii – ni muhimu kuhusisha jamii, kutoa elimu, kupata elimu ya wakazi wa eneo husika, na kujumuisha mitazamo yao. Uhifadhi bila jamii hauwezekani.”

Lucia alihitimu shahada yake ya sayansi ya wanyamapori na uhifadhi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, mwaka 2020. Mbeleni, Lucia anapanga kufanya shahada yake ya uzamili kwenye yanja ya uhifadhi, hasa kwenye masuala ya uhusiano kati ya jamii na spishi zilizo hatari, mfano tembo na tai.

Vai (kushoto) na Lucia (kulia) wakitafiti kiota cha tai katika mapori ya akiba ya Ikorongo – Grumeti, wakiwa na msaidizi wao  Mahmoud (katikati). 

Vainess na Lucia ni wawakilishi wawili tu, wa washiriki mahiri wa programu ya WIF. Programu ya wanawake kwenye uhifadhi itaendelea kuwawezesha wanawake wa kitanzania kukabliliana na changamoto kwenye kuwa na mchango wenye matokeo chanya na wenye maana kwenye kazi za uhifadhi na tafiti. Kwa mitazamo yao kwenye sekta hii, washiriki wa programu ya WIF watasaidia uhifadhi wa baadaye kuwa jumuishi, wenye ubunifu na wenye usawa.

Kwa kushirikiana na washiriki wa WIF, kama Vainess na Lucia, Grumeti inatumai kutengeneza viongozi wa baadaye kwenye uhifadhi wanaovunja mipaka kwa yale yanayowezekana kwa vijana, na kusimama mstari wa mbele kwa wanawake Tanzania.

Kuchangia kwa ajili ya programu ya wanawake kwenye uhifadhi bofya hapa.  

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia