Zaituni, Faru yatima

Zaituni ni mojawapo ya hadithi za mafanikio tunazopenda kusimulia kuhusu faru mweusi wa Mashariki. Zaituni, ameonyesha ukuaji tangu alipopatikana yatima kwa mara ya kwanza katika uwanda wa Serengeti mwishoni mwa mwaka 2019. Serikali ilimkabidhiwa Zaituni kwa Grumeti Fund kusaidia kumtunza na, tangu wakati huo, timu yetu ya uhifadhi, pamoja na washirika wetu wa serikali TAWA na wadau kama TAWAIRI na TANAPA, wamefanya kazi hii bila kuchoka kumlinda na kumtunza.

Vikundi vya walinzi waliojitolea wanafanya doria katika eneo la Grumeti muda wote. Mafanikio haya ya pamoja yasingekuwepo bila wao. Wanaume kwa wanawake wanaojitolea maisha yao kumtunza Zaituni na faru wengine wa Mashariki ni muhimu. Mmoja wa wafanyakazi waliojitolea ambaye amekuwa na Zaituni tangu alipofika ni Mzee Dickson. Mzee Dickson amekuwa na Zaituni tangu alipofika kwa ajili ya uangalizi ambapo wanasayansi walikadiria kuwa alikuwa na umri wa miezi minne hadi mitano.

Ni maajabu tunayoyaona kwa Zaituni. Alikuja hapa akiwa mdogo sana na dhaifu. Tulikuwa tukimfunika kwa blanketi na kulazimika kumkumbatia ili kumpa joto. Sasa ananawiri na anafurahia maisha.” – Mzee Dickson

Zaituni anapenda kujigaragaza kwenye tope. Sasa anajitafutia chakula chake na ameachishwa kunyonya maziwa. Sote tunafurahi sana kumuona akibadilika kuwa faru anayejitegemea na kutarajia kumuachia huru porini atakapokuwa tayari.

Uhifadhi wa wanyamapori ni operesheni ya pamoja. Pale ambapo tunajizatiti tukiungwa mkono na aina nyingine za uimarishaji wa usalama ndani ya hifadhi ya Ikorongo/Grumeti – ni muhimu kufanya kazi kwa pamoja na washirika wetu wa serikali kulinda ikolojia ya Serengeti.

Grumeti Fund imejitolea kuendeleza programu zinazosaidia uhamishaji na urejeshaji wa aina mbali mbali za wanyamapori walio katika hatari ya kutoweka katika jamii, Grumeti na kwenye ikolojia ya Serengeti kwa upana wake.

Kwa kushirikiana na washirika na wadau wetu, tunaangalia njia mbalimbali za kupata faru wa ziada ili kuharakisha mpango wa kuongeza faru weusi na kutoa mchango muhimu katika uhifadhi wa faru Serengeti.

Kuchangia uhifadhi wa faru weusi wa Mashariki walio hatarini kutoweka, bonyeza hapa.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia