Utunzaji wa serengeti ya magharibi
Wakati athari za janga hili la kimataifa likiwalimemetatiza maisha ya watu kwa kiasi kikubwa, kupungua na mtiririko wa ulimwengu wa asili unabaki bila mabadiliko. Na hivyo, kazi yetu ya kulinda ekari 350,000 za magharibi mwa Serengeti inaendelea. Kwa kweli, kutokana na kuzorota kwa shughuli za kiuchumi katika jamii jirani na kuanza kwa uhamaji mkubwa, tulitarajia ongezeka la ujangili. Kwa hiyo, kupata eneo hili kumekuwa ni jambo muhimu zaidi, na Idara ya Kupambana na Ujangili ya Grumeti Fund inaendelea kufanya kazi bila kuchoka kufanya eneo hili na wanyamapori wake salama – pamoja na kuwepo janga la kimataifa.
Hata hivyo,kitengo cha doria ya idara ya Kupambana na Ujangili kimekuwa kipengele muhimu katika kufanya mahali hapa kuwa salama. Kitengo hiki kikiwa na pikipiki, vifaa na mahema yasiyoonekana kirahisi na kusaidiwa na nishati ya jua, kinatembea kwa urahisi na kinajitegemea. Timu hii ya askari wa hifadhi 21 inaweza kusambazwa kwa siri katika vikundi vya watu wanne hadi sehemu yoyote katika eneo la hifadhi wakati wowote. Siyo tu kwamba wanaweza kuchukua eneo kubwa zaidi na kutumika kama kizuizi kwa wawindaji haramu, lakini Kitengo cha Doria (Mobile Patrol Unit)pia kina wasaa wa mwitikio wa haraka ambao unahakikisha uzuiaji kisi siri wa shughuli za ujangili.
Grumeti Fund inaamini kuwa kuzuia tukio la ujangili siku zote ni bora kuliko kuwakamata majangili ambao tayari wameua mnyama. Lakini, isingewezekana kuwazidi maarifa wawindaji haramu na kulinda eneo lote la hifadhi bila msaada wa timu yetu katika Kituo cha Operesheni ya Pamoja(JOC). Timu yetu ya JOC husaidia kutambua njia zetu za Kitengo cha Doria (MPU) na kuhakikisha kuwa rasilimali zetu zinatumika kwa njia ifaayo. Kwa kufanya doria zilizopangwa mapema na za kushitukiza, mchana na usiku, timu hii hulinda eneo la hifadhi vizuri ziaidi.
Usalama tunaohakikishwa na Idara ya Kupambana na Ujangili unaturuhusu kuanza na kujikita katika miradi kabambe kama vile uanzishaji upya wa faru weusi. Kwa mfano, hivi karibuni tulishuhudia kuzaliwa kwa mtoto wa faru – ndama wa kwanza wa faru mweusi wa Mashariki katika eneo hilo kwa miaka mingi- na tunatumai kuona zaidi. Grumeti Fund na washirika wetu wa serikali ya Tanzania, wanaendelea kutegemea kwa kiasi kikubwa juhudi zetu za ushirikiano, teknolojia na taarifa za kiintelijensia kwa pamoja ili kulinda na kuhifadhi ikolojia ya Serengeti.
Kuunga mkono juhudi za askari wa hifadhi na juhudi zetu za kupambana na ujangili, unaweza kubonyeza hapa kuchangia.