Kutoka Serengeti hadi Ziwa Victoria na Zaidi: Umuhimu wa Uhifadhi wa Mito kwa Ajili ya Wanyamapori na Jamii

Maji ni uhai na mstakabali wa viumbe hai ikiwa ni pamoja na binadamu hutegemea maji. Vyanzo vya maji vikiharibiwa au kuchafuliwa madhara yake huenda mbali zaidi.

Mito miwili, Grumeti na Rubana – hupita kwenye mapori yetu ya akiba ya Ikorongo – Grumeti yenye mkubwa wa ekari 350,000 Magharibi mwa Serengeti na kustawisha maisha ya viumbe hai ndani ya maeneo haya. Mito hii huishia kupeleka maji ziwa Victoria – ziwa la pili kwa ukubwa ulimwenguni ambalo ni chanzo cha maji kwa maelfu ya wakazi Afrika Mashariki. Mito hii inakabiliwa na vitisho vinavyoongezeka kila siku kutokana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na shughuli za binadamu na ongezeko la watu kwenye vyanzo na mapito yake. Kushindwa kulinda mito hii kutaathiri sio tu wanyamapori, bali na maisha ya binadamu pia.

Washiriki wakichukua sampuli na kutambua viumbe wa majini kwenye mto Grumeti ili kuweza kutambua ubora wa maji.

Kwa kutambua hitaji hili la haraka RISE na Idara yetu ya Utafiti na Ufuatiliaji imezindua mpango muhimu wa kufuatilia na kulinda mazingira ya maji ya mito hii ndani ya eneo letu la uhifadhi. Kwa kuelewa afya ya mito yetu tunaweza kuchukua hatua za uhifadhi wa haraka ili kuhakikisha uhai wake.

Kuimarisha juhudi zetu za uhifadhi Joshua Benjamin mwanafunzi wa PhD ya Zoolojia kutoka Chuo Kikuu cha Florida alijiunga nasi pamoja na wataalam wengine kuongoza semina ya mafunzo ya siku sita kati ya tarehe 24 Februari na 2 ya Machi. Prof Charles Mwithali Merimba kutoka Chuo Kikuu cha Egerton huko Kenya Laban Njoroge na Dk. Lulu Kaaya kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma walifanya kazi na sisi kutoe elimu hii kwa watafiti wa Tanzania, wahifadhi na wahitimu wa vyuo vikuu juu ya ustadi muhimu wa kutathmini ubora wa maji kwa kutumia wadudu – viumbe ambavyo vinaonyesha ubora wa maji. Kwa kuwapatia wataalamu hawa mafunzo juu mbinu hizi zisizo na gharama kubwa tunaiwezesha jamaa kuwa wasimamizi wa vyanzo vyao vya maji.

Changamoto hii sio tu barani Afrika – bali mazingira ya maji safi ulimwenguni sio mazuri. Huko Marekani mito kama Mississippi na Colorado inakabiliwa na vitisho vya uchafuzi wa mazingira, matumizi mabaya na uharibifu wa maskani. Ulimwenguni kote ubora wa maji unadhoofika kwa sababu ya taka za viwandani, ukataji miti na mabadiliko ya hali ya hewa. Haja kuchukua hatua ni ya uharaka pasipokujali mahali tunapoishi.

Timu yetu ya utafiti na ufuatiliaji kwa kushirikiana na RISE inachukua hatua ya uhifadhi wa maji safi ya muda mrefu. Kwa kutumia viumbe hai wa majini kutathmini ubora wa maji tunaweza kufuatilia mabadiliko kwa wakati na kutoa ufahamu muhimu wa kuongoza juhudi zetu za uhifadhi. Ili kufanya kazi hii kwa ufanisi iwezekanavyo tunahitaji zana sahihi za ufuatiliaji. Logger ya Tathmini ya Maji ya Steelhead itaturuhusu kufuatilia mifumo muhimu ya mto kwa usahihi, kukusanya data kwa wakati halisi ambayo itatusaidia kwenye mikakati ya uhifadhi.

Unaweza kuwa sehemu ya misheni hii kwa kutusaidia kupata zana hii muhimu na kufanya athari ya kudumu kwenye uhifadhi wa mito. Tunahitaji kupata $ 14000 kufadhili mradi huu. Ikiwa unavutiwa tafadhali bonyeza hapa kuchangia na kulinda njia hizi za maji kwa vizazi vijavyo!

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia