Kuimarisha Jitihada Zetu dhidi ya Ujangili

Mitego ya nyaya na vikundi vikubwa vya biashara ya nyamapori vinabaki kuwa tishio kwenye juhudi zetu za uhifadhi. Vikundi hivi vya biashara haramu sio tu husambaza nyamapori ndani ya maeneo ya hapa karibu lakini pia huuza nje ya mipana, hivyo kuweka shinikizo kubwa kwa wanyama wa porini katika mazingira ya mfumo wa ikolojia ya magharibi mwa Serengeti.

Kushughulikia changamoto hizi kunahitaji zaidi ya teknolojia; inahitaji timu iliyojitolea na kujizatiti. Ndio maana mwezi ujao tutawakaribisha vijana 44 wenye nguvu kutoka jamii za pembezoni na maeneo yetu ya hifadhi kujiunga na timu yetu ya kukabiliana na ujangili.

Skauti hawa wapya wataongeza nguvu kwenye doria, kutawala maeneo ya hifadhi kwa miguu na kuleta nguvu mpya na ujuzi katika mapambano dhidi ya ujangili. Uwepo wao utaongeza uwezo wetu wa kujibu haraka vitisho na kuturuhusu kuzingatia maeneo muhimu na yenye changamoto kubwa.

Kuanzia Januari 5 askari hawa walianza programu ya mafunzo ya siku tatu iliyolenga kuwaandaa kwa jukumu kubwa lililo mbele yao. Miongoni mwa mafunzo hayo ni Pamoja na ukakamavu wa mwili, matumizi ya silaha, ufatiliaji, mbinu za doria, ujanja wa porini, na ujuzi muhimu wa matibabu.

Glen Steyn, meneja wetu wa Idara ya kupambana na Ujangili anasisitiza umuhimu wa misheni hii: “Lengo letu ni kulinda na kuhifadhi bayonuai wa mfumo wa Ikolojia wa Magharibi wa Serengeti kwa vizazi vijavyo. Kazi hii ni ngumu na mara nyingi ni hatari, lakini tunabaki imara tukiazaimia kulinda wanyama wa porini na makazi yao.”

Asante kwa mchango wako endelevu, tumefanya maendeleo makubwa katika miongo miwili iliyopita. Kwa pamoja tumeokoa wanyama wengi kutoka kwenye mitego ya nyaya, kuwatibu wanyamapori waliojeruhiwa, kufanya doria za mchana na usiku na kuwezesha jamii za wenyeji na njia mbadala za kiuchumi.

Tunapoendelea na kazi hii muhimu mwaka huu 2025 tunakualika usimame nasi. Ungana nasi kwenye dhamira yetu ya kulinda wanyamapori  na kuhakikisha mustakabali mzuri kwa kizazi kijacho.

Bofya hapa kuwa sehemu ya uhifadhi wa wanyamapori leo!

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia