Kutambulisha programu ya BizRaiz

Grumeti Fund imejitolea kufanya kazi na jamii za wenyeji zinazozunguka eneo hili la hifadhi ili kutengeneza fursa za kuzalisha kipato kupitia mpango wa maendeleo ya biashara. Tangu kutekelezwa kwake, mpango wa Enterprise Development Programme umefanikiwa kutoa mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 900 kupitia programu zake za Village Learning and Guiding Programme inazingatia mbinu ya moja kwa moja ya kubadilisha mitazamo na kujenga uhusiano na wajasiriamali wa ndani, ambapo programu hii elekezi inazingatia  msaada wa kina wa biashara ya mtu mmoja-mmoja.

Mwaka jana, Grumeti Fund na mshirika wake Raizcorp waligundua kuwa kuna hitaji muhimu la huduma za ziada ili kuziba pengo kati ya programu za Village Learning and Guiding. Kwa hiyo, programu ya BizRaiz ilianzishwa. Lengo la programu hii ni kutoa fursa kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa wahitimu kutoka Village Learning ambao wameanzisha biashara zao lakini bado hawajawa tayari kuingia katika programu ya Guiding – kimsingi, kuendelea “kuinua biashara”.

Mafunzo ya BizRaiz hufanyika mara moja kwa wiki kwa dakika 90 kwa miezi mitatu mfululizo katika vijiji vinavyozunguka wilaya za Bunda na Serengeti. Wajasiriamali kumi na wawili wamechaguliwa kutoka kila kijiji kinachoshiriki. Wakati wa mafunzo kila mjasiriamali huwa na kipindi cha dakika 45 kutoka kwa Afisa Miradi wa Grumeti Fund, na kufuatiwa na mjadala wa kikundi wa dakika 45 kuhusu changamoto na uzoefu wao.

Nyamase Mangari Nyitika ni miongoni mwa washiriki hai wa mpango wa BizRaiz katika Kijiji cha Mugeta kilichopo wilayani Bunda. Akiwa mjasiriamali na mama wa watoto watatu, Nyamase alianza biashara yake ya ushonaji mwaka 2019 na cherehani moja na pesa za Kitanzania shilingi 50,000 (takriban dola za Kimarekani 20). Baada ya kuhitimu programu ya Village Learning, Nyamase alihisi bado anahitaji msaada kutoka kwa Afisa Mradi wake wa Grumeti Fund.

Biashara yangu bado haikuwa shwari nilipohitimu Village Learning Programme. Ilikuwa changamoto kuiimarisha lakini nilibaki kuwa na mtazamo chanya na mwenye matumaini huku nikitumia mafunzo niliyopata kutoka kwa Village Learning Programme kukuza biashara yangu. Mwaka 2020, nilifanikiwa kununua kiwanja ambapo nilijenga ofisi yangu, niliweza kuongeza cherehani moja zaidi na kuanza kuuza vitambaa vya kisasa kwa wateja wangu. Nilipopokea simu kutoka kwa Afisa Mradi wa Grumeti Fund kuhusu mpango mpya wa BizRaiz, nilifurahi sana na nilijua kwamba nilikuwa hatua moja karibu kufikia ndoto zangu za kukuza biashara yangu.

Mwishoni mwa Februari 2021, programu ya BizRaiz ilianza na kuleta matumaini mapya kwa wajasiriamali wa ndani chini ya uwezeshaji wa Afisa Mradi mpya Pamela Selasini.

Nawashukuru Grumeti Fund kwa kunisajili katika programu hii. Ninajifunza na kufanya mazoezi ya njia za kusimamia na kukuza biashara yangu kila siku. Mambo muhimu zaidi kuhusu kipindi hiki ni kubadilishana uzoefu na fursa ya kutumia mbinu tunazojifunza. Mrejesho wa kila wiki ni muhimu. Sikuwahi kufikiria kupanua biashara yangu. Faida niliyopata niliitumia kutunza familia yangu na kusomesha watoto wangu. Vipindi hivi vimenifundisha kuweka akiba na nimeweza kufungua akaunti ya akiba katika benki yangu. Nimejifunza kutafuta na kujaribu fursa mpya, kwa mfano sasa nina mwanafunzi wa ushonaji ambaye amesaidia kupanua biashara yangu.” – Nyamase Mangari Nyitika

Kwa sasa Nyamase amesajili biashara yake baada ya kutiwa moyo na afisa wake wa Miradi, Pamela.

Mtaji wake wa biashara umeongezeka kutoka pesa za Kitanzania shilingi 50,000 (takriban dola za Kimarekani 20) na wateja 6 kwa mwezi hadi pesa za Kitanzania shilingi 350,000 (takriban dola za Marekani150) na kuhudumia hadi wateja 20 kwa mwezi.

‘’Bado nahudhuria programu ya BizRaiz. Wiki hii tulijifunza kuhusu jinsi ya kuongeza wateja na umuhimu wa mrejesho wa wateja. Kila wakati nakuwa na shauku ya mafunzo yetu ya kila wiki. Lengo langu mwaka huu ni kuongeza wateja zaidi kwa kupata habari za mitindo na vitambaa vya kisasa mapema. Ningependa kuajiri mtu mwingine na kuongeza wanafunzi wa ushonaji pia”. – Nyamase Mangari Nyitika

Mnamo 2021, mpango wa maendeleo ya biashara kupitia BizRaiz unalenga kufikia watu 144 katika vijiji 8.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia