Samani rafiki kwa mazingira, RISE

Tulipokuwa tunafikiria jinsi kituo – kilichokusudiwa kukuza utafiti wa hali ya juu wa uhifadhi na kushughulikia changamoto nzito za uhifadhi zinazoathiri mfumo wa ikolojia  Serengeti – unavyopaswa kuwa, tulijua kwamba muundo unaojali ulimwengu ndiyo njia sahihi. Kwa hiyo, mnamo Juni 2020, tulipokamilisha ujenzi wa RISE, kituo chetu kipya cha utafiti ambacho kina vipengele muhimu vya miundo endelevu kama vile nishati ya jua, uvunaji wa maji ya mvua na utumiaji wa nyenzo za asili, tulifurahi. Hata hivyo, tulitaka kwenda mbele zaidi. Tuliwasiliana na wauzaji wengi wa ndani wanaojali mazingira, na biashara za kijamii kadri tulivyoweza ili kuweka samani katika jengo hili. Haya ni majina na biashara tulizoziunga mkono:

Dunia Designs 

Sisi hapa Grumeti tunajivunia wapiganaji wa One Planet na kwa ujumla tunajaribu kuepuka matumizi ya plastiki, tukichagua nyenzo zinazotunza mazingira kila inapowezekana. Lakini, katika hali isiyozuilika ambapo tuna taka za plastiki, sisi hurejesha kila mara kupitia Dunia Designs – kampuni ya usanifu rafiki kwa mazingira inayojikita katika utumiaji upya na bora wa chupa za plastiki, mifuko ya plastiki na nyenzo nyingine zilizochakatwa ili kuunda samani zinazostarehesha. Shukrani kwa uhusiano huu unaoendelea, tuliweza kupata seti nzuri ya sofa kwa ajili ya nafasi ya ubunifu na sanamu ya mamba kwa ajili ya chumba cha kulala wageni huko RISE. Dunia designs si tu kwamba wanageuza takataka kuwa hazina; bali pia wanajitolea kuelimisha vijana, kuajiri watu wa ndani (hasa wanawake) na kuandaa biashara nyingine na malighafi inayojali ardhi.

Shanga 

Shanga ni mshirika wetu mwingine wa One planet – Tumekuwa tukitayarisha taka za bilauri nao kwa miaka mingi. Shanga ni biashara inayojali mazingira, na ya kijamii inayojitolea kuajiri watu wanaoishi na ulemavu. Kwa miaka 13 sasa, biashara hii ya kijamii imeunda vito vya kipekee, vya hali ya juu, vilivyotengenezwa kwa mikono,  vyombo vya kioo na vifaa vya nyumbani ambavyo vinajumuisha vifaa vilivyotengeneza kutokana na taka. Bidhaa za Shanga zinauzwa nchini Tanzania, na duniani kote, huku faida ikirudishwa katika kuendeleza fursa za kuajiri watu wengi zaidi wanaoishi na ulemavu. Taa katika chumba cha ubunifu, shada la taa za mapambo na vyombo vyote vya bilauri RISE vinatoka Shanga.

WomenCraft

Kuongeza nakshi na muonekano wa rangi kwenye bafu huko RISE ni urembo wa mapambo ya ukuta kutoka WomenCraft. WomenCraft ni biashara ya ndani iliyosajiliwa na Fare Trade katika Wilaya ya Ngara sehemu ya vijijini kaskazini-mashariki mwa Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2007, WomenCraft imeongeza fursa za kiuchumi baada ya vita, eneo la mpakani mwa Rwanda, Burundi na Tanzania kwa kuwaleta pamoja wanawake wa vijijini, kuwezesha ukuaji wao na kuunganisha ujuzi wao na soko la kimataifa. Kupitia WomenCraft, zaidi ya mafundi 600 wanajiendeleza, wanatunza familia zenye nguvu, huchangamsha jumuiya zao na kuutia moyo ulimwengu unaowazunguka.

Inaya Zanzibar

Timu ya uzalishaji Inaya Zanzibar wote wakiwa wanawake ilitoa sabuni na mafuta yatumikayo bafuni. Yametengenezwa kutokana na mimea, mafuta na viambata vya Kiafrika vilivyochaguliwa kwa umakini kwa ajili ya matumizi, panapowezekana, viungo vya kaboni na vilivyovunwa porini. Bidhaa za Inaya ni za kifahari na rafiki wa mazingira. Kilichotuvutia kwa Inaya, ni ukweli kwamba bidhaa zao zimetengenezwa kwa mikono, zimeunganishwa kwa mkono, zinamiminwa kwa mikono, na zimefungwa kwa mikono katika vikundi vidogo ili kuhakikisha hubaki kwenye ubora wake, uchafuzi wa kiwango cha chini na viwango vya ubora wa hali ya juu.

Starfish Pottery

Vyombo vya mfinyanzi vilivyopo RISE vimetengenezwa kwa mikono Arusha. Bidhaa za Starfish Pottery huchakatwa kwa gurudumu na hutengenezwa kwa mikono kutokana na udongo wa mawe yanayopatikana nchini. Biashara hiyo inamilikiwa na wanawake na inazalishwa kwa makundi madogo madogo wakitupa taka kidogo sana au hata bila kutupa taka yoyote.

The Green Room 

RISE pia ina benchi ya meza ya nje iliyowekwa kutoka Green Room. Seti hiyo imetengenezwa kwa mbao zilizobuniwa na mafundi wa ndani. Mkusanyo wa vitu vyote kutoka The Green Room vimeundwa na kuzalishwa jijini Dar es Salaam, lakini pia kujumuisha bidhaa kutoka zaidi ya biashara nyingine 40 za ufundi nchini Tanzania na kwingineko. Pia wanashirikiana na mashirika mengi ya misaada na mashirika ambayo wanasaidia kupitia mauzo ya bidhaa zao. The Green Room wanazalisha bidhaa nzuri, za kupendeza ambazo pia zinawajibika kijamii na kimazingira.

Zaidi ya kununua mapambo yanayojali mazingira, pia tuliamua kufanya kazi na kuwapatia mafunzo fundi seremala wa ndani kutengeneza baadhi ya samani hapa hapa. Kwa kutumia mbao zilizoidhinishwa na FSC, seremala wa ndani walitengeneza meza na sehemu zote za kufanyia kazi.

Wakati samani zetu nyingi tumezinunua ndani ya nchi huifanya RISE kuwa jengo endelevu tulilotarajia – kulingana na maadili ya kiujumla ya mipango ambayo itasimamia – pia hutusaidia kuwa waungwana na kudhamiria kuendeleza jamii za wenyeji. Biashara nyingi za ndani, haswa zile zinazotegemea utalii, zimeathiriwa vibaya na UVIKO19 kwa hiyo manunuzi yetu, ingawa ni madogo sana, yamesaidia biashara hizo kuendelea kuwepo wakati wa nyakati hizi za majaribu.

Iwapo umeguswa kusaidia biashara hizi, tunakuhimiza kufanya hivyo. Bonyeza hapa

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia