Awamu ya mwezi na msimu hubadilisha matumizi ya barabara na simba

Muhtasari.

Barabara ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa hurahisisha usimamizi na utalii lakini pia zinaweza kubadilisha mienendo ya wanyama na fursa za kutafuta chakula. Nyayo za wanyama zinazoonekana kando ya barabara pia hutumiwa kuorodhesha mgawanyiko na wingi wa spishi. Tulichunguza mchango wa barabara kwenye mienendo ya simba (Panthera leo) ndani ya mfumo wa ikolojia wa Serengeti nchini Tanzania. Tulitumia vioneshi vya maeneo ya kila saa kutoka kwa simba 18 wenye kola za GPS ili kukadiria athari za muda wa muda (diel, lunar, and seasonal) na ukubwa wa eneo kwenye matumizi ya barabara na simba na marudio ya kuvuka barabara katika kipindi cha 2018-2019.

Matumizi na kuvuka kwa Barabara kati ya mchana na usiku hayakutofautiana lakini yalitofautiana kati ya 63% wakata wa mwezi angavu na 82% kati ya misimu. Matumizi makubwa ya simba barabarani na matukio ya kuvuka barabara wakati wa kiangazi na mwangaza mwingi wa mwezi unaweza kuhusishwa na kupungua kwa malisho kwa sababu mawindo ya simba hayapatikani sana wakati wa kiangazi na hupatikana kwa kiwango cha chini cha mafanikio wakati wa kuangaza zaidi kwa mwezi. Kwa vile matumizi ya barabara ya simba yalitofautiana kati ya misimu na awamu ya mwezi tunapendekeza uzingatiaji wa tofauti hizi wakati wa kuorodhesha idadi ya simba kwa kutumia data inayotokana na tafiti zinazotumia barabara kama njia za kupita. Soma makala kamili.

Waandishi

Stanslaus B. Mwampeta

Lusato M. Masinde

Peter S. Ranke

Eivin Røskaft

Robert Fyumagwa

Jerrold L. Belant.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia