Kulinda Wanyamapori Mchana na Usiku

Wakati wa mapambazuko wakati sehemu kubwa dunia wakiwa wamelala, kundi la watu lililojitolea  linaingia kazini. Ni saa 11:30 asubuhi na maskari wetu wa Idara ya uzuiaji ujangili wanajitayarisha kwa ajili ya ratiba yao ya kila siku ya mazoezi ya viungo. Ratiba yao si ya watu lelemama—inahusisha mazoezi makali kama kukimbia kilomita tatu na uzito wa kilo 10 mkononi pamoja na mamia ya mzoezi ya viungo kama vile, sit-ups na pushups. Mashujaa hawa wanafanya haya mazoezi makali kwa muda wa saa moja lakini ni mwanzo tu wa dhamira yao ya kulinda wanyamapori wanaoishi kwenye ekari 350,000 za mapori yetu ya akiba. Karibu kwenye mstari wa mbele wa uhifadhi, ambapo ari, nguvu, na shauku hukutana ili kulinda wakazi wa sayari yetu walio hatarini zaidi.

Kujituma kwao na ustadi usioyumbishwa, timu yetu ya skauti hupita bila woga katika maeneo yenye changamoto nyingi, hisia zao zikifuata kikamilifu ishara za shughuli haramu zinazohatarisha wanyamapori wetu wa thamani. Wanasimama kama walinzi, wakiwa tayari kuchukua hatua kwa haraka wakitetea wanyamapori chini ya ulinzi wao makini.

Mfano wa matokeo ya kujitolea kwao ulijidhihirisha mwezi uliopita tu, wakati askari wetu sita wakiambatana na maskari watatu wa Kitengo cha K9 na maskari wawili wa TAWA, walilifanikiwa kumkamata jangili akiwa na  nyama pori. Jua likiwa kali, majira ya saa 7:00 mchana, lakini misheni yao ilikuwa bado haijakamilika. Baada ya kumpata jangili huyo walimpeleka kituo cha polisi Serengeti ambapo taratibu za kisheria zilikuwa zinawasubiri. Hii ni pamoja na kushughulikia kwa uangalifu ushahidi na utoaji wa taarifa zote za kina ili kuhakikisha mwindaji haramu anakabiliana na haki.

Siku ikielekea kuwa jioni na uchovu ukitishia kuanza, Pampu kiongozi wao Hodari wa timu alipokea simu ya dharura ya kijasusi kutoka kwa Kabichi. Taarifa za tukio jingine la ujangili katika kijiji jirani cha Wilaya ya Serengeti ziliwahitaji muitikio wao wa haraka. Bila kusita, walikimbia hadi kijijini na kuanzisha operesheni usiku mzima ambayo ilifanikisha kukamatwa kwa jangili mwingine aliyekutwa na nyama pori kwenye makazi yake. Usiku huohuo walimsafirisha jangili huyo hadi kituo cha polisi kilichokuwa karibu kwa ajili ya taratibu zaidi za kisheria.

Wakiwa wameshinda walirudi hifadhini alfajiri, dhamira yao ya kazi yao ikathibitishwa maradufu. Kupitia doria zisizokoma za mchana na usiku wanatambua na kupunguza hatari zinazoweza kutokea kwa wanyamapori wetu na kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu wa mfumo wa ikolojia wa Serengeti.

Unapounga mkono timu yetu ya kupambana na ujangili unakuwa sehemu muhimu ya jitihada za kulinda wanyama walio hatarini kutoweka kama vile faru weusi wa mashariki na kuzuia shughuli haramu kama vile ujangili. Kwa pamoja tuna uwezo wa kuleta athari kubwa katika kuhifadhi bioanuwai wa mfumo huu wa ikolojia unaopendwa, kuulinda kwa ajili ya kufurahia vizazi vijavyo. Mchango wako sio tu zawadi; ni urithi wa uhifadhi ambao utaonekana siku zote.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia