Kukabili mustakabali wa Elimu
Uhifadhi endelevu unamaanisha kuinua na kuwezesha jamii zinazozunguka eneo la Grumeti. Idara yetu ya mahusiano ni muhimu katika kuhakikisha tunajenga uhusiano wa maana wa kudumu kwa muda mrefu na jamii ambazo zimekuwepo hapa kwa enzi kabla yetu na zitakazokuwa hapa miaka mingi baada yetu. Kuinua na kuelimisha jamii zinazotuzunguka ni muhimu katika kufanya uhifadhi kuwa endelevu.
Tunaambiwa kuwa elimu ndio ufunguo wa mafanikio, hapa Grumeti tunaendelea kuthibitisha kupitia elimu kuwa mabadiliko chanya yanaweza kutokea. Moja ya malengo yetu makubwa ni kubadilisha maisha ya kila siku ya jamii zinazozunguka eneo hili.
Tumedhamiria kuwa elimu itafika kila pembe ya Tanzania. Serikali ya Tanzania imehakikisha kila kata na kijiji nchini kinakuwa na shule ya msingi na elimu ya msingi bila malipo. Grumeti Fund inaendelea kuunga mkono juhudi hizi za elimu kwa kusaidia pale panapowezekana.
Kijiji cha Singisi chenye takriban wakazi 3000, kiko mkabala na eneo la Grumeti. Shule ya msingi ina wanafunzi wapatao 800 kutoka kijiji cha Singisi na Motukeri wanaosoma, lakini ni jengo moja tu lililo katika hali nzuri lililojengwa mwaka 2002; shule ya msingi ilijengwa mwaka 1974.
Pamoja na elimu kuwa bure siku hizi, changamoto ni kuwatengenezea wanafunzi na walimu mazingira salama ili waweze kustawi, si tu kutaka kuweka mazingira salama wa majengo, bali kuna changamoto za kuwa na walimu wa kutosha wanaojituma na wenye sifa stahiki, vifaa vya kufundishia, vifaa vya kisasa, milo bora, na hata madawati ya kutosha.Changamoto hizi huwakatisha tamaa wazazi wengi kuwaleta watoto wao shuleni na kutofanya vizuri kitaaluma.
Tulipoanza marekebisho ya shule ya msingi Singisi mwaka 2021, madarasa yalikua hayana sakafu ya saruji, wanafunzi walikua wakikaa kwenye tofali chini, kuta za darasa zilikua karibu kuanguka, na ilikua sehemu isiyofaa kabisa kwa watoto kuwepo.
Moja kati ya watu wazima katika kijiji cha Singisi, anaefahamika kama Mzee Christopher, aliyekuwa sehemu ya waliojenga hii shule ya msingi mwaka 1974, alisema:
“Mfuko wa Grumeti umesaidia kubadili Maisha ya vijiji vingi vya jirani, na sasa shule ya msingi katika Kijiji chetu. Tuonapo hili kama wanakijiji, tunakuwa na ujasiri wa kubadili mitazamo yetu kuhusu uhifadhi.
Baadhi yetu tulikua majangiri kipindi cha nyuma, ambao hatukuelewa uhifadhi ni nini kabla ya Mfuko wa Grumeti kuja na kutufundisha sisi na Watoto wetu.”
Tulipoanza ukarabati wa shule ya msingi ya Singisi mwaka 2021, madarasa hayakuwa na sakafu ya zege, wanafunzi waliketi kwenye matofali sakafuni, kuta za darasa zilikuwa zikianguka, na kwa kweli hapakuwa mahali wezeshi kwa watoto.
Mmoja wa wazee anayefahamika kwa jina la Mzee Christopher katika kijiji cha Singisi ambaye alikuwa sehemu ya timu iliyojenga shule ya msingi mwaka 1974, anasema.
Grumeti Fund imesaidia kubadilisha vijiji vingi vya jirani, na sasa shule ya msingi katika kijiji chetu. Tunapoona haya sisi kama wanakijiji, tunakuwa na ujasiri wa kubadilisha mitazamo yetu kuhusu uhifadhi. Baadhi yetu zamani tulikuwa ni wawindaji haramu, ambao hawakuelewa uhifadhi ni nini kabla ya Grumeti Fund kuja na kutuelimisha sisi na watoto wetu.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Vicent Okworo (Katika picha hapo juu) anasema, “hatupokei tu wanafunzi kutoka kijijini kwetu bali pia kutoka vijiji vinavyotuzunguka. Kwa majengo haya ya kisasa, tunatarajia kuwa na mahudhurio mazuri na ufaulu wa juu. Mwaka jana shule yetu kwa ufaulu ilikuwa ya 31 kati ya shule 100 wilayani. Tunaamini kwa kweli tutashika nafasi ya juu zaidi mwaka ujao, na tunaishukuru Grumeti Fund kwa wema wao kukarabati shule.”
Baadhi ya madarasa mapya ya shule ya msingi Singisi
Leo baada ya miaka 47, wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Singisi watasomea katika madarasa ya kisasa na salama yatakayowawezesha kusoma bila kuathiriwa na aina yoyote ya hali ya hewa.
Kwa wahisani wote waliofanikisha hili kwa michango yao, tunaendelea kuwashukuru na kuwaomba muendelee kusaidia programu zetu za elimu za Grumeti Fund.