Grumeti Fund

Grumeti Fund ni Shirika lisilo la faida linalochangia kuhifadhi Ikolojia ya
Serengeti kwa vizazi vijavyo.

TAZAMA VIDEO KAMILI

Kazi zetu

Sehemu nyingi ulimwenguni zinapoendelea kuharibika kutokana na ongezeko kubwa la watu, Grumeti Fund kwa kushirikiana na washirika wetu wa Tanzania inajizatiti katika kuhifadhi ekari 350,000 za eneo la Magharibi mwa Serengeti zilizopuuzwa hapo awali. Kupitia usimamizi dhabiti wa uhifadhi, kushirikiana na jamii, ubunifu wa teknolojia na kutumia askari mahiri tunaleta mabadiliko chanya na matokeo endelevu ya uhifadhi.

Ripoti ya Matokeo 2023

“Mafanikio endelevu ya uhifadhi wa maeneo ya magharibi mwa Serengeti ni matokeo ya pande mbili ya kulinda wanyamapori na kuboresha maisha ya jamii za pembezoni mwa maeneo haya.”

Pakua

Miradi muhimu

Mafanikio ya kazi za uhifadhi na kuboresha maisha ya jamii za pembezoni zinazofanywa na Grumeti Fund hutegemea uhisani wa wafadhili. Mchango wako utasaidia kuendelea kuhifadhi maeneo haya muhimu ya Ikolojia ya Serengeti na kusaiidia maendeleo ya jamii za pembezoni.

Changia

Habari Mpya

Fuatilia baadhi ya nyakati zetu nzuri zaidi za nyuma ya pazia na endelea kuhabarika na Habari zetu mpya na baadhi ya makala zenye taarifa kedekede hapa chini.

  • Kutoka Serengeti hadi Ziwa Victoria na Zaidi: Umuhimu wa Uhifadhi wa Mito kwa Ajili ya Wanyamapori na Jamii

    Maji ni uhai na mstakabali wa viumbe hai ikiwa ni pamoja na binadamu hutegemea maji. Vyanzo vya maji vikiharibiwa au kuchafuliwa madhara yake huenda mbali zaidi. Mito miwili, Grumeti na Rubana – hupita kwenye mapori yetu ya akiba ya Ikorongo – Grumeti yenye mkubwa wa......

  • Ng’ombe kwa Uhifadhi

    Vipi kama Ng’ombe wa maziwa huweza kubadilisha maisha? Hiki ndicho kinachotokea kwenye vijiji 21 vinavyopakana na mapori yetu ya akiba ya Ikorongo – Grumeti. Kupitia mradi wetu wa ng’ombe bora wa maziwa ulioko chini ya programu ya Climate-Resilience and Improvement Program (CLIP) sio tu tunalinda......

  • Kuimarisha Jitihada Zetu dhidi ya Ujangili

    Mitego ya nyaya na vikundi vikubwa vya biashara ya nyamapori vinabaki kuwa tishio kwenye juhudi zetu za uhifadhi. Vikundi hivi vya biashara haramu sio tu husambaza nyamapori ndani ya maeneo ya hapa karibu lakini pia huuza nje ya mipana, hivyo kuweka shinikizo kubwa kwa wanyama......

Makala zaidi

Washirika wakuu

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia