Victoria Mkessa

Mratibu wa Programu

Victoria Mkessa, MSc, ni mwanasayansi wa uhifadhi kwenye hatua za awali za taaluma, mwenye nia dhubuti katika dhana za jenetiki ya uhifadhi na matumizi ya utafiti wenyekutumika kuboresha maisha ya jamii. Alipata shahada yake katika Usimamizi wa Uhifadhi wa Mifumo ya Kiafrika kutoka Chuo Kikuu cha Glasgow, ambapo alisoma uhusiano kati ya twiga na wadudu wanaowasumbua katika mfumo wa Ikolojia wa Tarangire – Manyara. Vicky kwa sasa anafanya kazi kama Mratibu wa Programu kwa programu ya utafiti unaotumika ya Grumeti Fund, yaani, Utafiti na Ubunifu kwa Mfumo wa Serengeti (RISE). Katika jukumu hili, yeye huandaa na kupanga logistiki za programu, huwezesha programu za mafunzo kama “Women in the Field,” husaidia katika utafiti wa mijongeo ya tembo kwa muda mrefu na utafiti wa kuweka kamera, na anaendelea kukuza na kufuatilia mapenzi yake binafsi ya utafiti.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia