Kristen Denninger Snyder, PhD

Mwanasayansi Kiongozi
Mwasayansi Mtafiti, Colorado State University

Kristen ni mwanasayansi wa uhifadhi ambaye daima amekuwa akivutiwa na kusoma wanyamapori na ulimwengu wa asili. Uzoefu wake wa utafiti wakati wa shahada yake ya kwanza na wakati mwingi uliotumika kutembelea Hifadhi za Taifa na maeneo ya pori katika Magharibi mwa Marekani uliibua shauku yake ya kufanya kazi kwenye uhifadhi. Kristen alipata Shahada ya Uzamivu ya Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha California – Davis, ambapo utafiti wake ulilenga migogoro kati ya binadamu na wanyamapori na mipango ya uhifadhi. Migogoro na kuishi kwa pamoja kati ya binadamu na wanyamapori bado ni kipaumbele katika kazi yake, ambayo anashughulikia kutoka mitazamo mbalimbali na kutumia zana mbalimbali, ikiwa ni pamoja na tafiti za kaya, kamera, kola za GPS za wanyamapori, na uchunguzi wa kutumia rimoti.

Kristen alijiunga na Grumeti Fund mwaka 2015 wakati anamalizia shahada yake, na baadaye alijiunga na timu kama mwanafunzi baada ya shahada yake kwa kushirikiana na Wittemyer Lab katika Chuo Kikuu cha Colorado State. Sasa kama Kiongozi wa Sayansi, Kristen anaongoza programu ya Utafiti na Ubunifu kwa ajili ya Mfumo wa Serengeti (RISE). Sehemu anayopenda zaidi katika kazi yake ni kuweza kufanya kazi kila siku kujenga daraja kati ya sayansi na uhifadhi huku akisaidia kuwafunza kizazi kijacho cha wanasayansi wa uhifadhi nchini Tanzania.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia