Kent Greenawalt

Mtazamaji

Kent S. Greenawalt ni Mwenyekiti na Mkurugenzi mtendaji wa Foot Levelers, wasambazaji namba moja wa vifaa vya mifupa. Pia Kent ni mbobezi wa muda mrefu wa utaalamu wa matibabu ya mifupa, na muasisi wa taasisi ya mchakato wa oparesheni za mifupa, ambayo imejizatiti kuelimisha juu ya faida za matibabu ya mifupa.

Kama mvumbuzi, mfadhili na mfanyabiashara, Kent ametengeneza na kulesinisha dazani za bidhaa za afya na kutoa msaada endelevu kwenye vyuo vya matibabu ya mifupa, tafiti na taasisi binafsi na kupitia Foot Levelers. Tuzo za heshima za Kent hujumuisha Udaktari wa Heshima wa oparesheni za mifupa kutoka chuo cha mifupa cha Cleveland.

Mwaka 2001, Kent alikusanya zaidi ya dola za Kimarekani $ 600,000 kwa ajili ya wahanga wa shambulio la 9/11 na jitihada zingine za kutoa misaada. Miaka minne baadaye, aliweza kusaidia tena kuleta zaidi ya dola za Kimarekani $ 600,000 kwa ajili ya usafi na mradi wa kupunguza makali ya maisha baada ya Kimbunga Katrina kuharibu Orleans Mpya. Huko Foot Levelers’ nyumbani kwa Roanoke, Virginia, Kent ametumikia kwenye bodi ya Roanoke Symphony, Bustani ya wanyama ya mlima Mill, makumbusho ya sanaa ya Taubman na taasisi ya mafanikio ya watoto ya Kusini-magharibi mwa Virginia.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia