David Mwakipisile

Meneja Mahusiano

David amekulia Tanzania akiwa na Imani ya kuwa tuliumbwa kuishi pamoja na Wanyama. Kama Meneja wa Mahusiano wa Grumeti Fund, anao uwezo wa kutekeleza suluhu ambazo uhifadhi na maendeleo ya jamii huja pamoja ili kusaidia watu na wanyamapori kuishi kwa usalama.

Kazi ya David inalenga kusaidia jamiii kutatua changamoto ngumu kama vile migogoro baina ya binadamu na wanyamapori, kuimarisha uhusiano wao na mazingira, na Grumeti Fund, pamoja na kudumisha na kujenga ubia na usimamiaji wa pamoja na wadau mbalimbali wa serikali ya Tanzania na kusaidia utekelezaji wa maradi mbalimbali ya uhifadhi.

David ana shahada ya Sayansi ya Usimamizi wa Wanyamapori kutoka Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine. Aliungana na Grumeti Fund mwaka 2014 na kabla ya kuwa Meneja wa Mahusiano mwaka 2020, ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya Usimamiaji wa Uhifadhi na Uzuiaji-Ujangiri, kulikopelekea kupata uelewa wa kina wa idara zingine ndani ya shirika. Kabla ya kuwa Sehemu ya Grumeti Fund, David amefanya kazi katika maeneo ya hifadhi nchini Tanzania na taasisi za serikali kama vile TANAPA, TAWA na Wizara ya Maliasili na Utalii.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia