Kwa kushirikiana na idara nyingine, Idara ya miradi maalumu hufanya kazi kama kichochezi cha nguvu kati ya Grumeti Fund. Kutambulisha teknolojia mpya na mbinu za kibunifu za uhifadhi, uzuia-ujangiri na tafiti na ufuatiliaji, kuwezesha shirika kupata matokeo mazuri na ya uhakika kuleta yenye mafanikio makubwa.
Miradi maalumu iliyowekwa hujumuisha kitengo cha mbwa, DAS, ndege zisizokuwa na rubani, kamera za siri za TrailGuard na uwekwaji wa kola za GPS kwa tembo. Miradi mingine chini ya Idara ya miradi maalumu ni programu ya Grumeti Fund ya uongezaji wa faru weusi, utambulishaji mpya wa tandala mkubwa na programu muhimu ya msaada wa anga.