Ilikuweza kufahamu vizuri mifumo ya kiikolojia katika eneo husika, na kuweza kupima ufanisi wa kazi zetu za kijamii na uhifadhi, tunawekeza kikamilifu kwenye programu za utafiti na ufuatiliaji kwa lengo la kuboresha kumbukumbu za muda mrefu za mabadiliko ya vigezo muhimu.
Timu yetu ya ufuatilia mazingira, kiwango cha kaboni kwenye udongo, mzunguko wa maji, kiwango cha uoto na hali ya spishi, moto, spishi vamizi (wanyama na mimea), idadi ya wanyama wakubwa, spishi kubwa na muhimu za ndege na migogoro ya binadamu na wanyamapori. Programu ya kisasa ya ramani za GIS huwasaidia kuweka alama kwa usahihi kwenye kila kitu kuanzia mioto pori na uvamizi wa mimea vamizi hadi migogoro ya binadamu na wanyamapori na matukio ya ujangiri. Hizi taarifa huongoza maamuzi yetu.