Ufikiaji wa jamii

Grumeti Fund imefanikiwa kutengeneza na kuzindua programu ya UPLIFT (Unlocking Prosperous Livelihoods for Tomorrow) yaani Kufungua Maisha Yenye Mafanikio ya Kesho). Hii ni programu ya kufikia jamii yenye kusudi la kuboresha maisha ya jamii pembezoni mwa mapori haya ya akiba. Katika maeneo ambayo asilimia kubwa ya wakazi wake hutegemea kilimo kuingiza kipato – kazi ambayo ina kabiliwa na changamoto nyingi kama vile mabadiliko ya tabia nchi na wanyama vamizi mashambani hususani tembo – Grumeti Fund huwajengea wakazi uwezo, nyenzo na rasilimali zinazowawezesha kujikimu kwa ujumla. UPLIFT hutumia mitazamo mitatu endelevu kuboresha maisha ya jamii hizi: kuwasaidia vijana kupata viwango vya juu na bora vya elimu; kuongeza fursa za kuongeza kipato; na kuhamasisha kuishi na wanyamapori kwa amani.

Elimu

Grumeti Fund husaidia kuboresha elimu kwa vijana kwenye jamii za wenyeji ili kuwawezesha kupata maarifa na ujuzi unaotakiwa maishani. Msaada hutolewa katika mfumo wa uhisani kwa shule za sekondari, vyuo vya ufundi na elimu katika sekta ya uhifadhi na utalii.

Ili kupata uzoefu wahisaniwa huwa na waangalizi/washauri kutoka Grumeti Fund, hupatiwa mafunzo ya stadi za maisha na fursa za mafunzo kazini katika shirika.

Kwenye mfumo wa elimu wa Tanzania, lugha hubadilika ghafla kutoka Kiswahili kwenye shule za msingi kwenda Kiingereza kwenye shule za sekondari, na hili hukwamisha uwezo wa wanafunzi wengi kufanya vizuri kitaaluma. Hivyo, Grumeti Fund hushirikiana na Concordia kutengeneza kambi za lugha zenye lengo la kuwezesha stadi za Kiingereza kwa wanafunzi wa shule za msingi kupitia vipindi vya kambi vya kila mwaka.

Kumuwezesha mtoto wakike ni kipaumbele katika programu zote za elimu za Grumeti Fund. Makongamano ya kumuwezesha binti hufanyika kila mwaka, na mada kadha wa kadha kama vile uwezeshaji, afya, ujasiri, na ukuaji na balehe huzungumzwa.

GRUMETI FUND
Grumeti Fund

Ukuzaji wa Biashara

Sambamba na operesheni za kutokomeza ujangiri wa wanyamapori zinazofanywa na Idara ya  utekelezaji wa sheria ya Grumeti Fund, ni muhimu kuwa na njia mbadala za kuingiza kipato kusaidia familia zilizokuwa zikitegemea kazi ya ujangiri kujikimu. Grumeti Fund imeungana na Raizcorp – wataalam wa biashara wenye rekodi nzuri za kukuza biashara.

Programu ya ukuzaji wa biashara imegawanyika katika sehemu kuu mbili: Uangalizi na Madarasa vijijini. Uangalizi ni mbinu ya kukuza biashara ambayo hujumuisha mtu-na-mtu (Mwalimu na Mwanafunzi), hii huwawezesha wajasiriamali kuimarisha stadi za ukuzaji wa biashara, wakati Madarasa vijijini imeundwa na vipindi vya kila wiki ambavyo wajasiriamali vijijini hufundishwa juu ya stadi za biashara na maendeleo binafsi.

Soma zaidi

Kituo cha elimu ya mazingira

Lengo la Grumeti Fund kwenye elimu hujumuisha mazingira na wajibu wa kila mtu kuweza kupunguza madhara kwenye mazingira yetu. Kwenye Kituo cha Elimu ya Mazingira (EEC), wanafunzi kumi na mbili wakiongozwa na mwalimu wao hujifunza mambo muhimu ya kimazingira kama vile ukataji wa misitu, mmomonyoko wa udongo na uhifadhi wa maji ambavyo uathiri kila mmoja.

EEC

Mafanikio

330
Wanafunzi kupitia vijiji vya lugha grumeti

92
wajasiriamali waliofundishwa kupitia programu ya ukuzaji wa biashara ya raizcorp

582
Watoto wakike waliojihusha kwenye matukio ya uwezeshaji mwaka 2017

100+
Ufadhili unaotolewa kila mwaka

Tazama taarifa ya matokeo
Language Immersion Camp

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia