Grumeti Fund ni shirika lisilo la kutengeneza faida linalojishughulisha na kazi ya uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya jamii katika ukanda wa Ikolojia ya Magharibi mwa Serengeti nchini Tanzania.
Ndoto yetu ni kuwa na ulimwengu ambao binadamu na wanyamapori huishi pamoja kwa uendelevu, siku zote.
Hadi sasa, zaidi ya wafanyakazi mia moja sitini na tano hulinda, husimamia na kuangalia pori tengefu la Grumeti ambalo hapo awali yapata miaka 20 iliyopita halikuwa na wanyama, na sasa limefurika wanyamapori tena. Ari na kujitoa kwao kunasukumwa na historia na kuongozwa na taswira pana.