Tofauti za kijinsia katika uwiano wa miili ya twiga wa Kimasai na mabadiliko ya shingo ya twiga

Wandishi:

Douglas R. Cavener, Monica L. Bond, Lan Wu-Cavener, George G. Lohay, Mia W. Cavener, Xiaoyi Hou, David L. Pearce & Derek E. Lee

Muhtasari

Twiga huonyesha utofauti mkubwa wa kijinsia katika saizi ya mwili. Ikiwa mabadiliko ya jinsi pia yapo katika uwiano wa mwili wa mifupa ya axial na appendicular imejadiliwa hasa kuhusu shingo ndefu ya twiga. Tulichunguza uwiano wa anatomiki wa shingo, miguu ya mbele na nyuma, na shina la mwili wa twiga wa Kimasai (G. tippelskirchi) katika kundi lilo porini na walio kwenye mashamba ya wanyama. Tuligundua kuwa twiga majike wa Kimasai wana shingo ndefu sawa na miguu yao ya mbele kuliko madume kinyume na nadharia ya asili ya shingo kwa ngono ambayo ilipendekeza kuwa mabadiliko ya shingo ndefu ya twiga yalipelekewa na ushindani baina ya madume. Hata hivyo, upana wa shingo ya madume na uzito unaoonekana ni mkubwa kwa uwiano kuliko majike; na kuunga mkono nadharia ya shingo-kwa-jinsi. Zaidi ya hayo, urefu wa mguu wa mbele wa dume ni mrefu zaidi wakati urefu wa kiwiliwili cha jike ni kirefu zaidi.

Tofauti hizi za kijinsia zilionekana kwa twiga wa Kimasai walio kwenye mashamba ya wanyama na porini. Tunakisia kwamba mabadiliko ya awali ya shingo na miguu mirefu ya twiga yalitokana na ushindani wa kipekee na mahitaji ya chakula baina ya spishi tofauti na mahitaji ya twiga jike wakati wa ujauzito na kunyonyesha kupitia uchaguzi asilia “natural selection” ili kupata faida ya ushindani katika kula majani na kisha baadaye uzito wa shingo uliongezeka zaidi kama matokeo ya ushindani baina ya madume na uchaguzi wa kijinsia.

Tofauti katika uwiano wa vipengele vikuu vya mwili hufafanua phenotype za jinsia lakini twiga kadhaa huonyesha phenotypes za jinsia tofauti na kiwango cha juu zaidi cha utengano unaoonekana kwa madume yaliyoko kwenye zoo. Tunakisia kuwa utofauti wa uwiano wa kijinsia hudumishwa porini kwa uteuzi wa asili na/au wa kijinsia, lakini kwenye mashamba ya wanyama (zoo) hulegezwa na kusababisha kutokea kwa mtafaruku mkubwa kwenye phenotypes za kijinsia. Kusoma zaidi, bonyeza hapa

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia