Glen Steyn

Meneja Kupambana na Ujangili

Glen Steyn alijiunga na Grumeti Fund mwaka 2023 kama Meneja wa Kupambana na Ujangili. Glen alikuwa mwanachama wa Wanajeshi wa Kifalme wa Uingereza ambapo alihudumu mara nyingi nyingi kwenye opareshini za Mashariki ya Kati. Baada ya miaka sita katika Jeshi la Wanamaji la Uingereza aliamua kutumia ujuzi na utaalamu wake wa kijeshi ili kuendeleza ulinzi na uhifadhi wa wanyamapori. Glen amefanya kazi nchini Afrika Kusini, Namibia, Msumbiji, Zambia, na Cameroon katika kupambana na uhalifu wa wanyamapori na ujangili kama mshauri wa kukabiliana na ujangili. Akiwa na shauku na hamasa kuziwezesha timu za kimataifa za kupambana na ujangili na kujenga uwezo wao kwa uendelevu Glen ametoa mafunzo kwa wanaume na wanawake kote barani humo ambao huingia katika hali hatarishi na hatari kila siku ili kulinda wanyamapori kwa vizazi vijavyo. Lengo la Glen kwa Kitengo cha Kupambana na Ujangili cha Grumeti Fund ni kuendelea kukiongezea ujuzi kwa mafunzo ya kitaaluma na kuongeza kasi ya utendaji kazi ili kusaidia zaidi kulinda wanyamapori wa mfumo wa ikolojia wa Serengeti.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia