Paul Keating

Mkurugenzi

Paul Keating ni Mkurugenzi mkuu na mkuu wa idara ya uhisani wa Vulcan Inc. Katika nafasi hii, Paul huangalia potifolio ya ruzuku kwa Vulcan na taasisi ya familia ya Paul G. Allen. Hii hujumuisha uhifadhi wa wanyamapori, bahari, tabia nchi na programu za jamii, pamoja na miradi inayoshughulikia majanga mbalimbali yanayotokea (kama vile Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na UVIKO-19 huko Washington, USA). Awali kabla ya kujiunga na Vulcan mwaka 2017, Paul amefanya kazi kwa miaka 20 na Umoja wa Mataifa na kufanya kazi kwenye programu za kimataifa za maendeleo katika nyanja za maendeleo endelevu, maendeleo ya jamii, utatauzi wa migogoro, na na usaidizi wa kibinadamu. Katika majukumu hayo, ameishi na kufanya kazi Afrika, Mashariki na Kusini mwa Asia, pamoja na Marekani, Ulaya na Oceania, ikijumuisha New Zealand. Paul ana shahada ya uzamivu katika mahusiano ya kimataifa na masomo ya kimkakati, na shahada ya sheria na Sanaa. Ameoa na ana familia ya Watoto wawili.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia