Walter Kansteiner, III 

Mkurugenzi

Walter Kansteiner, III ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 ndani ya Afrika na mambo masoko mapya ya biashara. Kama mwanzilishi wa Kikundi cha Scowcroft anashauri mashirika kwenye masuala mapana ya muungano, upatikanaji na ubinafsishaji barani Afrika kwenye nyanja ya mawasiliano ya simu, misitu, madini, huduma za kifedha, huduma za afya na usafiri wa anga. Walter alitoa ushauri wa ubinafsishaji wa dola za kimarekani bilioni 1.3 wa Telkom ya Afrika Kusini, mpaka sasa ndio ubinafsishaji mkubwa Afrika.

Walter amekuwa katibu msaidizi wa taifa kwa masuala ya Afrika kwa muda wa miaka miwili, kwenye masuala ya sera za kigeni za Marekani barani Afrika. Pia alikuwa mwakilishi binafsi wa Rais kwenye machakato wa G8 Afrika. Awali kabla ya ushirika wake na Kundi la Scowcroft, Walter alikuwa makamu wa Rais mtendaji wa kampuni ya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa. Pia alitumikia serikali ya Marekani kama Mkurugenzi wa masuala ya Afrika kwenye Baraza la mambo ya Ulinzi wa Taifa. Alikuwa ni mtaalam wa Afrika kwenye upangaji wa sera ya Katibu wa Nchi, na mjumbe wa nguvu kazi ya mkakati wa madini akiwa na kitengo cha ulinzi. Ni mjumbe wa baraza la Uhusiano wa Kigeni, mwenyekiti wa jopo la ushauri wa sera Afrika (kundi la washauri wenye mamlaka), na pia hutumika kwenye bodi mbalimbali Marekani na Afrika.

Walter kapata shahada zake kwenye uchumi wa kimataifa na maadili kutoka chuo kikuu cha Marekani na chuo cha Theolojia na Seminari Virginia.

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia