Professor Hussein Sosovele
Mkurugenzi
Hussein Sosovele ana Udaktari wa filosophia kwenye sosholojia na usimamizi wa rasilimali, pamoja na diploma baada ya shahada kwenye usimamizi na makadirio ya kimazingira.
Sosovele ni Profesa katika Taasisi ya makadirio ya rasilimali, chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambapo hufanya tafiti, ukufunzi na kutoa huduma mbalimbali za kijamii katika usimamizi wa mazingira, udadavuzi wa sera, ulinzi wa sera za kitaifa na kimataifa, na usimamizi wa miradi.
Nje ya Tanzania, Sosovele ana uzoefu wa kina wa Afrika, amewahi kufanya kazi Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Malawi na Netherlands. Pia, Sosovele amefanya kazi na mashirika ya kimataifa, kama vile WWF Tanzania ambapo aliratibu programu mbalimbali za USAID na zile zilizo fadhiliwa na Ujerumani zinazohusiana na usimamizi wa wanyamapori na sera. Pia, Sosevele alikuwa na mchango mkubwa kwenye uundaji na usimamizi wa maeneo ya kijamii na wanyamapori nchini Tanzania, na kujihusisha kikamilifu kwenye uandaaji wa sheria mbalimbali za mazingira na wanyamapori nchini Tanzania.
Sosevele ni mshiriki wa Jumuiya ya Kimataifa ya Makadirio ya Madhara, Jumuiya ya Makadirio ya Madhara Afrika Mashariki, na mshiriki wa Kamati ya Kiufundi juu ya uchumi na maendeleo ya vijiji na makubaliano kwenye Uhifadhi wa ndege wa majini wahamao Afrika-Ulayaasia (AEWA). Pia ni mtaalamu wa makadirio ya mazingira aliyesajiliwa kulingana na sheria za Tanzania.
Zaidi ya muongo Profesa Sosovele, pamoja na Hifadhi ya Singita Grumeti na Grumeti Fund wameshirikiana katika miradi mbalimbali yenye tija kwenye uhifadhi endelevu, maendeleo ya utalii wa kiikolojia wenye mafanikio ya juu, kufungamanishwa uhifadhi endelevu na maendeleo ya jamii, Magharibi mwa Serengeti. Mwezi Februari 2015, Sosovele alikubali mwaliko wa kujiunga na bodi ya Grumeti Fund.