Mahusiano

Grumeti Fund inafanya kazi kudumisha, kujenga na kuimarisha mahusiano ya karibu na wadau wote wa karibu wa serikali, uhifadhi na jamii ya wenyeji zinazofanya kazi ndani ya Ikolojia ya Serengeti, hivyo kutuwezesha kufanya kazi yetu kwa ufanisi.

Hasa, tunafanya kazi kwa kushirikiana na Singita, ambayo hufanya kazi kwenye mapori yetu ya akiba; Kitengo cha Wanyamapori cha Wizara ya Maliasili na Utalii, mamlaka mbalimbali za serikali za wilaya na mikoa, mabaraza ya vijiji na mashirika mengine ya serikali na taasisi zisizo za faida.

Uhusishwaji wa mahakama

Mfumo wa mahakama ni muhimu kwenye kufanya kazi ya kupunguza uhalifu wa wanyamapori na shughuli nyingine haramu za uvunaji wa maliasili. Idara ya Mahusiano ya Grumeti Fund inafanya kazi kwa ukaribu na mahakama ya wilaya, wanamashtaka wa jamii na kitengo cha uzuia-ujangiri mkoani.

DSC_8687

Kupunguza migogoro ya binadamu na wanyamapori

Idara ya Mahusiano hufanya kazi kubwa kwenye kutatua migogoro ya binadamu na wanyamapori. Ikiwa katika kijiji kilicho mpakani mwa hifadhi kitengo cha utatuzi wa migogoro ya binadamu na wanyamapori hufanya kazi kwa ukaribu na chumba cha operesheni ya taarifa ili kuzuia na kukabili matukio ya migogoro ya binadamu na wanyamapori yanayotokea maeneo ya karibu.

Wadau muhimu wa ikolojia ya serengeti

Kazi tunayoifanya Grumeti Fund isingefanikiwa bila kushirikiana. Kwa bahati nzuri, tunasaidiwa na wadau jasiri wanaoshiriki ndoto yetu.

Kitengo cha wanyamapori
Mamlaka Ya Usimamizi Wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)
Hifadhi Za Taifa Tanzania (TANAPA)
Eneo La Usimamizi Wa Wanyamapori Ikona (WMA)
Maamlaka Ya Uhifadhi Wa Eneo La Ngorongoro (NCAA)
Maamlaka Ya Utafiti Wa Wanyamapori Tanzania (TAWILI)
Jamii Ya Mambo Ya Wanyama Frankfurt (FZS)

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia