Matukio mengi ya ujangiri Grumeti uhusisha ujangiri wa uuzaji wa nyamapori, ingawa, ujangiri wa tembo kwa ajili ya pembe uko palepale na unaweza kuongezeka. Grumeti Fund hujumuisha teknolojia pamoja na askari mahiri kudhibiti uwindaji huu wa pande mbili. Tumeweka kambi kumi na mbili za kudumu za askari wa doria na mtandao wa maeneo ya kutazamia mienendo ya majangiri hifadhini yanayokuwa na watu masaa ishirini na nne. Zaidi ya hayo, mtandao wa redio za kidijitali sambamba na kanzidata ya utekelezaji wa sheria uhakikisha kuwa rasilimali chache za Grumeti hutumika kikamilifu na kwa uhakika.