Uhifadhi

Hekari 350,000 za eneo la Grumeti huunda sehemu muhimu ya Ikolojia ya Serengeti. Zaidi ya kurejesha na kutunza mandhari hii, Grumeti Fund inafanya kazi na serikali, jamii za wenyeji na wadau wengine kwenye miradi mbalimbali ya uhifadhi, kuanzia kwenye utambulishwaji tena wa spishi za wanyama wa asili waliotoweka, kusimamia mioto porini, na kuondoa mimea vamizi.

Wildlife Reintroduction CM

Programu ya utambulishaji upya wa wanyamapori

Grumeti Fund imejitoa kutengeneza programu zinazosaidia uhamishwaji na utambulishaji upya wa idadi ya spishi za wanyamapori walio hatarini kutoweka, na wa asili waliokuwepo kwenye mapori ya Grumeti na kwenye Ikolojia ya Serengeti hapo awali.

Grumeti Fund hutafiti namna mbalimbali za kuweza kupata faru wa ziada ilikuweza kuchochea programu ya kuongeza idadi faru weusi na kuchangia uhifadhi wa faru ndani ya Serengeti.

Mradi wa utambulishaji upya wa Grumeti Fund uhusisha urejeshaji wa Tandala Mkubwa waliokuwa wakipatikana katika mapori ya akiba ya Grumeti. Kwa kupata idhini kamili kutoka serikalini hivi punde, shughuli hii ya uhifadhi yenye kusisimua hutegemewa kufanyika mwakani, kutegemeana na uhisani.

Soma zaidi

Usimamizi wa mimea vamizi

Mimea vamizi ni hatari kwa ikolojia ya asili (kwa mimea na wanyama). Miongoni mwa mimea vamizi hatari  kwenye hifadhi yetu na jamii za jirani ni Chromolaena (Mwani Siam), Opuntia ( Pricky Pear), Parthenium (Feverfew) na Tithonia (Alizeti ya Mexico). Hadi sasa tuna programu ya kupambana na mimea vamizi ndani ya hifadhi na baadhi ya vijiji vya jirani ili kuweza kuitokomeza na kuzuia kuzaliana kwake tena.

Grumeti Fund

Usimamizi wa moto

Moto ni sehemu muhimu ya Ikolojia ya Serengeti. Ni tukio linalotekea kiasili, na hutumika kama nyenzo muhimu kwenye uhifadhi na usalama wa wageni. Pindi zoezi hili lifanyikapo kwa wakati sahihi, kuchoma moto hupunguza majani marefu yaliyozeeka; na kupelekea kuongezeka kwa majani malaini na yenye virutubisho kwa wanyamapori. Moto pia huboresha mzunguko wa virutubisho aridhini, kupelekea malisho yenye lishe kwa wanyamapori. Mioto inayoanzishwa kinyume na sheria husimamiwa kwa uangalifu pia, ili kuzuia madhara yasiyotakiwa kwenye ikolojia.

Grumeti Fund
WILDLIFE WELFARE

Ustawi wa wanyamapori

Kuwatibu wanyamapori wenye majeraha yaliyosababishwa na wanadamu ni muhimu kwenye ikolojia ambayo mitego ya wanyamapori kwa ajili ya biashara ya nyamapori ni tishio la kawaida. Kupitia ushirikiano mzuri na Taasisi ya Tafiti za Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Grumeti Fund inakusudia kutibu wanyama wengi waliosababishiwa majeraha na binadamu kadri iwezekenavyo na kupunguza idadi ya wanyama ambao wangeweza kufa kutokana na majeraha.

Mafanikio

1000%
Ongezeko la idadi ya mbogo tangu 2003

4
Ongezeko zaidi la wanyama jamii ya swala

511
Hekari zilizo tibiwa mimea vamizi mwaka uliopita

                  

Tafadhali tambua kuwa unahamishwa kwenda kwenye kurasa ya Shirika la Uhifadhi na Jamii za Kiafrika, Inc.

Nchini Marekani, Grumeti Fund ni mradi unaosaidiwa-kifedha na Shirika la Uhifadhi na jamii za Kiafrika, Inc. (“ACCF”), shirika la kimsaada 501(c) (3). Michango yenye kutozwa kodi kwa ACCF hutolowa kwa Grumeti Fund kusaidia kazi yetu.

Bonyeza hapa kuchangia